Historia ya Vita vya Majimaji inaonesha kuwa awali walikamatwa machifu 48 na baadaye kukamatwa wengine ambapo idadi ya machifu walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja ilifikia 66.
Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ni eneo ambalo limehifadhiwa vizuri na serikali ili kuwawezesha watu kujifunza kumbukumbu nyingi ambazo ni kivutio adimu cha utalii wa kishujaa na kiutamaduni. Watu kutoka mkoa wa Ruvuma na nje ya nchi wanatembelea eneo hili maarufu katika historia ya Tanzania hasa katika harakati ambazo zilifanywa na babu zetu kupambana na wakoloni ili kujitawala wenyewe bila kunyonywa. Mkurugenzi wa makumbusho ya Taifa ya Majimaji mhifadhi Kiongozi Balthazar Nyamusya anasema eneo hilo la makumbusho lina historia tatu ambazo ni historia ya vita vya majimaji,historia ya ujio wa wangoni kutoka Afrika ya Kusini na historia ya uhuru wa Tanganyika. Anaitaja historia ya vita vya majimaji ililenga kumkomboa mtanzania kutoka mikononi mwa wakoloni Wajerumani na kwamba sio sahihi kuwa vita hiyo ilikuwa na uwezo wa kugeuza risasi kuwa maji bali ililenga kuwapa nguvu wapiganaji kujitolea hata ikibidi kupot...









Comments
Post a Comment