Posts

Showing posts from October, 2022

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 23 OKTOBA, 2022

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa mara baada ya Rais huyo wa DRC kuwasili nchini tarehe 23 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix An

RAIS SAMIA NA RIPOTI YA KIKOSI KAZI MJADALA WA VYAMA VYA SIASA,UKATILI WA KIJINSIA NA RUSHWA

Image
kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa mujibu wa Katiba na Sheria pamoja na kuzingatia 40% ya jinsi katika vyombo vya maamuzi vya vyama vya siasa. Rais Samia ameunga mkono pendekezo la kufanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwani kutumia Sheria na Kanuni za awali zingeendelea kusababisha changamoto na dosari zilizokuwa zikijitokeza mwanzoni. Rais Samia pia amevitaka vyama vya siasa kutathmini mienendo ya vyama vyao hasa kuzingatia usawa wa kijinsia, matumizi mazuri ya fedha, utawala bora na kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa kuwawezesha wanawake kugombea nafasi muhimu. Vile vile, Kikosi Kazi hicho kimependekeza utaratibu mpya wa kupata Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, utendaji wa Tume uruhusiwe kuhojiwa kwenye Mahakama ya Juu na pia isilazimike kufuata amri ya mtu yeyote, Idara yoyote ya Serikali, Chama chochote cha siasa au Taasisi yoyote. Kikosi Kazi hicho chenye Wajumbe 24 na kilichowasilisha maeneo 9 ya kufanyiwa kazi, kimependekeza matokeo ya Uchaguzi wa Rais yahoj

RAIS SAMIA NA RIPOTI YA KIKOSI KAZI CHA KURATIBU MAONI YA WADAU WA DEMOK...

Image
“Nimesikiliza vizuri uwasilishwaji uliofanywa na Profesa Mukandala na nimesikiliza vifungu vyote alivyovisema.Vingine nilikuwa nasema ilo kweli? Lakini ni maoni ya kikosi kazi,”sio jambo la kukabidhiwa papo uanze kulifanyia kazi, lakini kikosi kazi kimependekeza mambo mazuri yanayotakiwa kuzingatiwa na kuyafanyia kazi katika utendaji wa Serikali.

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN APOKEA RIPOTI YA KIKOSI KAZI KUHUSU URATIBU MAONI YA WADAU WA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 21 OKTOBA, 2022

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022. Viongozi pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa P

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA SHIRIKA LA WANAWAKE KATIKA SHERIA NA MAENDELEO BARANI AFRIKA (WILDDAF) JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 20 OKTOBA, 2022

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa Tuzo baadhi ya Waanzilishi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika WiLDAF pamoja na vyeti kwa wadau waliofanikisha maendeleo ya Shirika hilo kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Shirika hilo kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa Tuzo baadhi ya Waanzilishi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika WiLDAF pamoja na vyeti kwa wadau waliofanikisha maendeleo ya Shirika hilo kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa

HOTUBA YA RAIS SAMIA NA MHE RAIS RUTO WAKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HAB...

Image

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AMEKUTANA NA MKE WA RAIS WA KENYA MAMA RACHAEL RUTO IKULU DAR ES SALAAM

Image
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amekutana na Mke wa Rais wa Kenya Mama Rachael Ruto Ikulu Dar es Salaam na kumzawadia mkufu na hereni zenye madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania pekee. Baada ya tukuo hilo Wake wa Marais hao walijumuika katika dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama  Samia Suluhu Hassan kwa mgeni wake Rais wa Kenya Mhe. William Ruto aliyekuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 📆 10 Oktoba 2022 📍Ikulu, jijini Dar es Salaam

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEKABIDHIWA RIPOTI YA KUCHAMBUA MAONI YA WASHIRIKI WA MKUTANO WA WADAU WA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA IKULU ZANZIBAR.

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Maoni ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Zanzibar,na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, hafla hiyo iliyofanyika  10-10-2022, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.  WAJUMBE wa Kamati Maalum ya (Kikosi Kazi) Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa kukabidhiwa Ripoti ya Kuchambua Maoni ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar 10-10-2022 na wa kwanza Mwenyekiti wa Kamati Maalum (Kikosi Kazi ) Dkt.Ali Uki na Makamu Mwenyekiti Mhe Balozi Amina Salum Ali. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum (Kikosi Kazi) wakati wa kukabidhiwa Ripot

MKUTANO WA WADAU WA DEMOKRASIA KUJADILI MASUALA MAHSUSI YA ZANZIBAR

Image
Demokrasia ni nini? Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya Umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile sheria na katika chaguzi. Wakati mwingine huwakilishwa na viongozi wao waliowachagua. Ni utawala wa watu, na watawala hutawala kwa ridhaa ya watu. Kwa hiyo kwa kifupi Demokrasia ni mfumo unatoa fursa ya madaraka kwa Umma moja kwa moja au kutokana na uwakilishi. Abraham Lincoln, Rais wa 16 wa Marekani, alisema Demokrasia ni serikali ya watu/mfumo wa utawala wa watu, kwa ajili ya watu na unaotokana na watu. Watu wanaunda serikali. Aina za demokrasia 1. Demokrasia ya moja kwa moja (kwa Kiingereza "Direct Democracy") ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, ya kijamii, ya kisheria na ya kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kam

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUJADILI MASUALA MAHSUSI YA ZANZIBAR YANAYOHUSU DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Wadau wa Kujadili Masuala Mahsusi ya Zanzibar Yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar tarehe 4-10-2022. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Wadau wa Kujadili Masuala Mahsusi ya Zanzibar Yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar tarehe 4-10-2022.   Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Kujadili Masuala Mahsusi ya Zanzibar Yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (haypo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo uliyofanyika katika ukum