MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AMEKUTANA NA MKE WA RAIS WA KENYA MAMA RACHAEL RUTO IKULU DAR ES SALAAM
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amekutana na Mke wa Rais wa Kenya Mama Rachael Ruto Ikulu Dar es Salaam na kumzawadia mkufu na hereni zenye madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania pekee.
Baada ya tukuo hilo Wake wa Marais hao walijumuika katika dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa mgeni wake Rais wa Kenya Mhe. William Ruto aliyekuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
📆 10 Oktoba 2022
📍Ikulu, jijini Dar es Salaam
Comments
Post a Comment