Posts

Showing posts from December, 2022

JE UNAJUA DELTA YA RUFIJI NDIO ENEO ZIMEZAMISHWA MELI KUBWA MBILI ZA KIVITA ZA UJERMANI?

Image
  Delta ya Rufiji. Picha kupitia panoramio.com © Bernd Zehring (https://ssl.panoramio.com/photo/802524 ) Kwa nini walikuwa wamekuja huku na walikuwa karibu kufanya nini? Washambulizi wa Biashara Baada ya kuanza Vita vya Kwanza vya Dunia, Jeshi la Wanamaji la Kifalme la Ujerumani lilikuwa na manuari nne zilizowekwa katika sehemu mbali mbali za ulimwengu. Meli hizi za kivita zilikuwa tishio kubwa kwa Uingereza  kufanya biashara na zilivuruga njia zote za bishara na usafirishaji lilikuwa jambo ambalo  Admiralty, Winston Churchill, kwa wazi alitaka kuliepuka.  Wanamaji wa SMS Karlsruhe na SMS Dresden walikuwa nje ya pwani ya mashariki ya Mexico; katika Pasifiki kulikuwa na kikosi chenye nguvu cha wanamaji, ambacho kilijumuisha SMS maarufu Emden, ambayo  ilianza safari ya ajabu na kusababisha hofu kubwa kwa meli katika Bahari ya Hindi. Wakati huo huo, pwani ya Afrika Mashariki kulikuwa na hii SMS Konigsberg. SMS Konigsberg jijini Dar es Salaam. mchoro na Ian Marshall. ©Ian Marshall / J. Rus

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA AFRIKA NA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA MASUALA YA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani (U.S Afirica Leaders Summit) wakati wakijadili masuala ya Kilimo, Usalama wa Chakula na Uzalishaji wa Chakula,  uliofanyika katika ukumbi wa Convention Centre Jijini Washington DC nchini Marekani tarehe 15 Desemba 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani  Mhe. Joe Biden pamoja na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika na Marekani kabla ya kuanza kwa ufungaji wa mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Convention Centre Jijini Washington DC nchini Marekani tarehe 15 Desemba 2022  

SHERIA INASEMAJE KUINGILIA KITU KISICHO KUWA CHAKO

Image

JE UMEWAHI KUJUA UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA?

Image
T ARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA  Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika. 1. WOSIA WA MAANDISHI Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja. Mtoa wosia asiye jua kusoma ua kuandika awe na mashuhuda wa nne wanao jua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia,mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja. 2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wa nne wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika. TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA SH

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azungumza katika Mkutano wa Uwekezaji na Wafanyabiashara wa Marekani Jijini Washington

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyabiashara wa Marekani kuhusiana na Sekta ya Uwekezaji nchini Tanzania katika Mkutano uliofanyika Jijini Washington DC nchini Marekani tarehe 13 Desemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mtendaji na Mkuu wa Mambo ya Kimataifa wa Chemba ya Biashara ya Marekani Myron Brilliant (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Marekani Dkt. Elsie Kanza (wa kwanza kushoto) kabla ya kuanza Mkutano wa Uwekezaji na Wafanyabiashara Jijini Washington nchini Marekani tarehe 13 Desemba, 2022.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Wakfu wa Big Win Philanthropy Jamie Cooper Jijini Washington nchini Marekani tarehe 13 Desemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Wakfu wa B