Posts

Showing posts from August, 2022

NINI KILITOKEA BAADA YA MAUAJI YA KIKATILI YA KIONGOZI MWANZILISHI WA D.R CONGO 🇨🇩 PATRICE LUMUMBA JANUARI 1961

Image
Tujikumbushe Dunia ilihamaki Baada ya mauaji ya kikatili ya Kiongozi mwanzilishi wa D.R Congo Patrice Lumumba Januari 1961, Waserbia walivamia ubalozi wa Ubelgiji katika mtaa wa Krunska wakipiga kelele mji mkuu wake Belgrade "Glory to Lumumba, death to Colonialism". Zaidi ya watu 80 walijeruhiwa siku hiyo huko Yugoslavia. Kifo cha Lumumba kilichochea maandamano katika balozi za Ubelgiji katika nchi kadhaa. Huko Belgrade, ubalozi wa Ubelgiji ulifutwa kazi na katika miji mingine, waandamanaji waliandamana na mabango wakisema "Uliua Lumumba, Wabelgiji!" Kinachosikitisha ni kwamba Patrice Lumumba aliomba msaada UN wakati wa uasi wa Jeshi na ukosefu wa usalama kutoka kwa vikundi vya waasi. UN haikuchukua hatua kwa wakati. Ubelgiji ilikuwa imetuma wanajeshi wake.tangu wakati huo hadi sasa DR Congo haijawana amani na vikosi vya walinda amani vipo Bado Waafrika wanapigana kugombea madaraka na Uporaji wa Rasilimali Lumumba anatufundisha Utawala wa sheria utatokana na ut

HISTORIA YA KUTUNGA KATIBA NA USHIRIKI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA. (SEHEMU YA PILI)

Image
TANU wakati h uo  ilifutilia mbali shirikisho la vyama vya wafanyakazi lililoitwa Tanganyika Federation of Labour (TFL) kwa kutunga sheria mpya National Union of Tanganyika Workers (Establishment) Act 1964.  Sheria hii pia ilianzisha shirikisho jipya la wafanyakazi. Athari bayana ya sheria hii ni pamoja na kuua uhuru wa vyama vya wafanyakazi nchini; na vyama vya wafanyakazi vilianza kuwekwa chini ya chama tawala na kufanya matawi ya TANU. Hili lilifuatiwa na kufutwa kwa vyama vya siasa vya upinzani mwaka 1965 na kuanzisha mfumo wa siasa wa chama kimoja.  Hapa katiba ya mwaka 1965 Ibara ya 3 ilitamka kuwa Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa chama kimoja na kuanisha kuwa TANU ndicho chama pekee kisheria Tanzania Bara na Afro-Shiraz Party (ASP) kiliendelea kuwa chama pekee huko Zanzibar.  Hii ni kufuatia muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa tarehe 26 Aprili 1964. Zaidi sana matakwa ya mfumo wa chama kimoja yalianisha kuwa masuala yote ya siasa mbali na yaliyoh

HISTORIA YA KUTUNGA KATIBA NA USHIRIKI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA

Image
  Historia ya chama cha siasa kuchukua jukumu kuu katika mchakato wa kutunga katiba (au hata kufanya marekebisho ya vifungu/vipengele vyake) unaweza kujadiliwa kuanzia mwaka 1961.  Ikumbukwe kuwa Tanganyika (sasa Tanzania) ilijipatia Uhuru wake mwaka huo toka kwa wakoloni wa Kiingereza kwa njia ya katiba iliyoruhusu “demokrasia” ya uwakilishi wa vyama. Hivyo baada ya chaguzi za kabla ya Uhuru, ni chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ndichokilishinda viti vyote   na kushika dola.  Katiba hiyo iliruhusu pia vyama vya kiraia kama vile vyama vya wafanyakazi, wanawake, na vijana kufanya shughuli zao. Lakini kutokana na lile lengo kuu la chama cha siasa kushika dola, TANU ilianza kujipanga na kuhodhi madaraka ya nchi hususani kwa kuanzisha sheria mpya.   TANU ilianza mradi mkubwa wa kutunga katiba mpya.Hapo Tanzania ikajikuta ikitunga katiba mpya kama nne:  Katiba ya Jamhuri (1962), Katiba ya Muungano (1964), Katiba ya Chama Kimoja (1965) na Katiba ya Kudumu (1977).

HISTORIA FUPI YA MUUNDO WA KATIBA WAKATI WA WAKOLONI HADI SASA

Image
  Ilitufikie malengo ya kutambua na kuelewa kwanini Katiba ni muhimu katika Nchi, yapaswa tujue Historia Pana ya Katiba na Sheria zeta kabla na baada ya Ukoloni  fuatana nasi Hapa kutambua  Katiba ya Watu ni ipi hasa Kwa ujumla nchi nyingi hasa zile zinazoendelea zina katiba zilizoandikwa.nyingi kati ya katiba hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka.Katiba hizo ni maridhiano ambayo yalilinda maslahi ya pande zote mbili: (1)Tawala za kikoloni zilizokuwa zikiandika. (2)Nchi iliyokuwa ikipata uhuru "Katiba nyingi katika nchi zilizoendelea zina uhusiano na Katiba na Tawala za kikoloni. Historia ya katiba hapa Tanzania pia ina uhusiano na tawala za kikoloni zilizokuwa zinatawala kabla ya uhuru  Historia Ya Mabadiliko Ya Katiba Tanzania 1961 Katiba ya kwanza ya uhuru iliyowekwa na Waingereza (Independence Constitution). Mwaka 1962 Katiba ya Jamhuri (The Republic Constitution) ili

SAFARI YA KATIBA NA UHURU WA TANZANIA YA LEO

Image
  Julai 7, 1954 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliongoza kikao cha Watanganyika 17 mjini (jijini) Dar es Salaam, kuanzisha chama cha kwanza cha siasa kilichoitwa “Tanganyika African National Union” (TANU). Kikao hicho kilimchagua Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa TANU. Alikuwa Rais pekee wa TANU mpaka mwaka 1977, TANU ilipoungana na ASP kuunda Chama Cha Mapinduzi au kwa kifupi CCM. Lengo la kwanza la TANU lilikuwa kuleta Uhuru wa Tanganyika na kazi ya kwanza ya TANU ilikuwa kuwatayarisha Watanganyika kwa kujitawala wenyewe. Harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Mwalimu Nyerere hazikuwa rahisi kwa sababu hiyo baada ya kupatikana uhuru, Nyerere aliitwa “Baba wa Taifa” ikiwa na maana ya mtu aliyeongoza juhudi za kutafuta uhuru na ujenzi wa Taifa jipya. Nyerere alijua fika sababu kwa nini mababu zetu hawakufanikiwa kukomboa nchi yao, kwani alikuwa mwanahistoria na alijua kuwa hakuwa mtu wa kwanza kuongoza juhudi za kutafuta uhuru. Wananchi wengi walitafuta uhuru kwa udi n

KATIBA YA NCHI NI NINI?

Image
Katiba ya Nchi ni nini? Katiba ya nchi ni muafaka wa kitaifa unaoanisha namna taifa linavyohitaji kujitawala katika mambo yote na kuendesha mambo yake. Hivyo basi, Katiba ya nchi ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali pia huanisha haki za msingi za wananchi. Katiba ya nchi hutungwa na wananchi wenyewe kama watu huru ili kupata muafaka wa taifa lao na namna gani wangependa kujitawala. Kwa kifupi, Katiba sio chombo cha wanazuoni wachache bali ni chombo kinachoonyosha umiliki wa nchi na rasilimali ya wananchi, nafasi ya 3 wananchi katika utawala na namna gani wangependa kuweka utawala wa nchi yao na hivyo kutengeneza muundo wa serikali yao. Kwa hiyo Katiba ya nchi ni waraka wa kitaifa unaoweka bayana, pamoja na mambo mengine, mfumo wa haki za msingi kwa wananchi wake, mihimili yake ya dola, namna ya kuweka utawala katika ngazi zote, muundo wa serikali yao na namna ya usimamizi wa mapata

KATIBA NI NINI ?

Image
  KATIBA ni sheria au kanuni zinazoaInisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao. Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi. Kuna aina kuu mbili za Katiba ambazo ni: (a) Katiba isiyo ya maandishi (ya kimapokeo) (b) Katiba ya maandishi. Inatajwa Katiba ya India ndiyo katiba ndefu kuliko katiba yoyote Duniani.