KATIBA YA NCHI NI NINI?
Katiba
ya Nchi ni nini?
Katiba ya nchi ni muafaka wa kitaifa
unaoanisha namna taifa linavyohitaji
kujitawala katika mambo yote na
kuendesha mambo yake. Hivyo basi,
Katiba ya nchi ni sheria mama
inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na
kuonyesha madaraka na majukumu ya
serikali pia huanisha haki za msingi
za wananchi. Katiba ya nchi hutungwa
na wananchi wenyewe kama
watu huru ili kupata muafaka wa
taifa lao na namna gani wangependa kujitawala.
Kwa kifupi, Katiba sio chombo cha
wanazuoni wachache bali ni chombo
kinachoonyosha umiliki wa nchi na
rasilimali ya wananchi, nafasi ya 3
wananchi katika utawala na namna
gani wangependa kuweka utawala
wa nchi yao na hivyo kutengeneza
muundo wa serikali yao.
Kwa hiyo
Katiba
ya nchi ni waraka wa kitaifa unaoweka bayana, pamoja na
mambo mengine, mfumo wa haki za
msingi kwa wananchi wake,
mihimili yake ya dola, namna ya
kuweka utawala katika ngazi
zote, muundo wa serikali yao na namna
ya usimamizi wa mapata
na matumizi ya rasilimali yote ya
kitaifa bila ukandamizaji wa aina
yeyote kwa jinsia zote
Comments
Post a Comment