Posts

Showing posts from July, 2023

MKUTANO WA KAMATI YA UONGOZI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA JULAI 31, 2023,

Image
  Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa mara baada ya kumaliza kikao cha kamati hiyo  jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Annamringi Macha, Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Juma Khatib na kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mzee John Momose Cheyo. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. (Picha na ORPP) Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vya Siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Momose Cheyo akichangia mada wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Uongozi

"UKABILIANAJI NA 'SEXTORTION' KATIKA VYUMBA VYA HABARI: WITO WA KUSIMAMA DHIDI YA GBV NA KUIMARISHA KUJIAMINI KWA WAANDISHI WA HABARI - DKT. ANNA HENGA"

Image
  "Ukabilianaji na 'Sextortion' katika Vyumba vya Habari: Kuongeza Ujasiri na Usawa kwa Waandishi wa Habari Wanawake - Hotuba ya Dkt. Anna Henga katika Mkutano wa WAN-IFRA Tanzania" Katika hotuba ya Dkt. Anna Henga wakati wa mkutano wa kujenga ujuzi na mtandao wa wafanyakazi wa zamani wa Women in News - WAN-IFRA Tanzania tarehe 28 Julai 2023 uliofanyika katika Hoteli ya Giraffe Beach jijini Dar es Salaam, alizungumzia suala la "sextortion" ambalo linawakumba waandishi wa habari katika vyumba vya habari.    Waandishi hawa wanadaiwa kushurutishwa kutoa miili yao ili kupata nafasi za kazi au vyeo. Baadhi yao wana ujasiri wa kukataa, lakini wengine wanajikuta wakiingia katika mtego wa ukatili unaotokana na jinsia (GBV) ambao pia unaathiri sana njia zao za kazi na kujiamini kwao.   "Sextortion" ni aina ya ukatili unaofanyika kwa kuwatishia au kuwahadaa waandishi wa habari, hasa wanawake, kwa kutumia madaraka yao ili kudhibiti kazi zao kwa kubadilishan

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 28,2023. SEHEMU YA NNE

Image
 KESI YA BANDARI TAREHE 28 JULAI 2023 Majaji wote watatu wanaingia saa 09: 44 asubuhi Tarehe 28 Juli 2023. MAJAJI WATATU; 1. Hon. Ndunguru 2. Hon. Ismail 3. Hon. Kagomba Wote wameinama wanaandika Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote. MAWAKILI WA SERIKALI; 1. Adv. Chang'a 2. Edson Mwaiyunge 3. Alice Mkulu 4. Stanley Kalokola 5. Edwin Lwebilo ... MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI; 1. Mpale Mpoki 2. Boniface MWABUKUSI 3. Philip Mwakilima 4. Livino Ngalimitumba. WALALAMIKAJI WOTE WAMEFIKA WAPO MAHAKAMANI 1. Alphonce Lusako 2. Emmanuel Chengula 3. Raphael Ngonde 4. Frank Nyarusi. Anasimama wakili wa serikali na kusema wako tayari kwa ajili ya REJOINDER kama hakuna pingamizi. Anasimama wakili senior Mpale Mpoki kwamba wako tayari na anaijulisha mahakama kwamba ataanza wakili msomi Boniface Mwabukusi kuwasilisha majibu yake. Atafuata wakili Msomi Livino na atamalizia Wakili Msomi Philip Mwakilima. Sasa anamkaribisha Wakili  Mwabukusi aendelee. Anasimama s

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. MWENDELEZO SEHEMU YA TATU

Image
Kesi Bandari majibu ya Upande wa Serikali SA Mayunge: Waheshimiwa majaji, Maamuzi ya Diana Rose Vs AG na alisemea viapo vya watu 72 havipo na walitakiwa kuleta viapo: Haya maamuzi yanategemea na maada inayobishaniwa. Na hoja yao ni suala la muda sio suala la idadi ya watu walioshiriki kutoa maoni. Tujikite kwenye  muda. SA Mayunge: Kwenye kiapo cha Maria, kwenye verification alisema haya anayoyasema, ni kwa ufahamu wake mwenyewe lakini pia 14.07.2023 tulifile kiapo cha Maria Mpale, kiapo hicho hakikupingwa na kimeeleza uwepo wa watu hao, maoni yalivyotolewa na kikaambatisha maelezo ya Bunge. SA Mayunge: Waheshimiwa majaji, kwenye annexure OSGAF5 ya Maria Mpale, kuanzia ukurasa wa 6 (Taarifa ya Bunge). Katika taaifa hiyo(anasoma;..)Sehemu hii inaeleza na kukiri  namna maoni yaliyopokelewa na Bunge kutoka kwa wadau yalivyosaidia na walalamikaji hawakupinga suala husika SA Mayunge: Waheshimiwa kwa upande wetu tumetekeleza mambo yote kwa mujibu wa sheria na hata hivyo walalamikaji hawakuzu

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA TATU

Image
TAREHE 27 JULAI 2023 MAJAJI WANAINGIA MUDA  SAA 09: 44 ASUBUHI. MAJAJI WATATU; 1. Hon. Ndunguru 2. Hon. Ismail 3. Hon. Kagomba Wote wameinama wanaandika Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote. MAWAKILI WA SERIKALI; 1. Adv. Mark Muluambo 2. Edson Mwaiyunge 3. Alice Mkulu  4. Stanley Kalokola 5. Edwin Lwebilo. MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI; 1. Mpale Mpoki 2. Boniface MWABUKUSI  3. Philip Mwakilima  4. Livino Ngalimitumba. Anasimama wakili kiongozi wa serikali Mr. Mark na kuijulisha mahakama kuwa wako tayari kuendelea na majibu yao. Mahakama inaruhusu. SA Kalokola: waheshimiwa naendelea na hoja namba 6 kama mkataba huu IGA ulizingatia sheria ya Manunuzi (Procurement Act) SA Kalokola: Hoja hii inatokana na ombi na 4 ya Origjnating summons kwamba IGA haikuzingatia Sheria ya Manunuzi. Na katika aya ya 12, walalamikaji wanasema kuna tender inetolewa kwa DP WORLD Kinyume na sheria za manunuzi. SA Kalokola: Majibu yetu yapo katika aya ya 14 ya kiapo cha  Moha

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA PILI

Image
  #Updates kesi ya bandari ---Sasa ni saa 14: 45 mchana Juli 26,2023 Majaji wanaingia,.. karani anataja namba ya kesi ambao ni kesi no.05/ 2023. ..Mahakama inakaa kwa utulivu kidogo huku majaji wakiandika. #Kesi_Ya_Bandari. Anasimama wakili wa serikali kuomba kuanza kujibu hoja za waleta maombi. SA = wakili wa serikali SA Mark : Waheshimiwa majaji W: Serikalin: Mark; waheshimiwa majaji naomba mahakama iangalie vitu gani vinapaswa kuangaliwa katika kesi ya kikatiba. Issue ya 1, 2 Edson atawalisha, issue 4,5 na 6 itawasilishwa na kalalokola, Edwin issue 3, Waheshimiwa maombi yameletwa chini ya ibara ya 108(2) ya Katiba ya Tanzania na Kifungu cha 2(3) cha JALA Kutumia Originating Summons na kiapo SA Mark: Kwa sasa tunaomba kibali cha mahakama tukufu ili majibu yetu na kiapo kinzani zitengeneze sehemu ya majibu yetu kinzani. Shauri hili linapinga uhalali wa kikatiba wa kutia sahihi na kuridhia mkataba wa kimataifa (IGA) baina ya nchi mbili. Tunawashukuru wenzetu kwa submission yao kwa sa b

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA KWANZA

Image
  KESI YA BANDARI  TAREHE 26TH JULY 2023 -----Majaji wanaingia  saa 09: 20----- MAJAJI WATATU; 1. Hon. Ndunguru 2. Hon. Ismail 3. Hon. Kagomba Wote wameinama wanaandika ----Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote. MAWAKILI WA SERIKALI; 1. Adv. Mark Muluambo 2. Edson Mwaiyunge 3. Alice Mkulu  4. Stanley Kalokola 5. Edwin Lwebilo MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI; 1. Mpale Mpoki 2. Boniface MWABUKUSI  3. Philip Mwakilima  4. Livino Ngalimitumba Anasimama wakili wa waleta maombi senior adv. Mpoki. Adv. Mpoki:  --Iwapendeze Waheshimiwa majaji tupo tayari kuendelea kwa utaratibu ufuatao. Nitatoa utangulizi na kuongelea kiini Na.2 Wakili Mwabukusi atazunguzmia issue no. 1 na 4. Msomi Livino atazungumzia issue na. 3 na Msomi mwakilima atazungumzia issue no.5 Bado anaendelea senior Mpoki. Adv. Mpoki Naomba nianze kwamba maombi haya yameletwa na walalamikaji 4 ambao wapo mbele yenu kwa mujibu wa ibara 108(2] ya Katiba ya Tanzania. Inayoipa mahakama mamlaka ya peke

NUKUU MUHIMU KUTOKA KWENYE HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU TAREHE 26 JULAI, 2023 JNICC – DAR ES SALAAM

Image
  TAHIMINI YA KINA YA HOTUBA HII INAONYESHA UMUHIMU WAKE KATIKA KUELEZEA CHANGAMOTO NA FURSA ZINAZOIKABILI AFRIKA NA JINSI YA KUTUMIA RASILIMALI WATU KULETA MAENDELEO ENDELEVU. HOTUBA HII INAONYESHA UFAHAMU MZURI WA HALI HALISI YA BARA LA AFRIKA NA INATOA MAPENDEKEZO YANAYOFAA KWA KUBORESHA HALI YA ELIMU, AFYA, NA MAFUNZO ILI KULETA MABADILIKO CHANYA NA USTAWI WA JAMII. Muhimu Zaidi: Ushirikiano : Hotuba hii inasisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, asasi za kiraia, na sekta binafsi katika kuleta maendeleo ya rasilimali watu. Ushirikiano huu unahitajika kwa ajili ya kuleta uwekezaji unaohitajika na kujenga mazingira wezeshi ya kukua na kuendelea kwa rasilimali watu.   Kuzingatia Demografia ya Vijana : Hotuba hii inaonyesha umuhimu wa kuutumia vizuri uwezo wa idadi kubwa ya vijana kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii. Inatoa wito wa kuchangamkia fursa ya "Demographic Dividend" kwa kuwekeza katika vijana na kuwapa ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.   Elimu na Maf