MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. MWENDELEZO SEHEMU YA TATU
Kesi Bandari majibu ya Upande wa Serikali
SA Mayunge: Waheshimiwa majaji, Maamuzi ya Diana Rose Vs AG na alisemea viapo vya watu 72 havipo na walitakiwa kuleta viapo:
Haya maamuzi yanategemea na maada inayobishaniwa. Na hoja yao ni suala la muda sio suala la idadi ya watu walioshiriki kutoa maoni. Tujikite kwenye muda.
SA Mayunge: Kwenye kiapo cha Maria, kwenye verification alisema haya anayoyasema, ni kwa ufahamu wake mwenyewe lakini pia 14.07.2023 tulifile kiapo cha Maria Mpale, kiapo hicho hakikupingwa na kimeeleza uwepo wa watu hao, maoni yalivyotolewa na kikaambatisha maelezo ya Bunge.
SA Mayunge: Waheshimiwa majaji, kwenye annexure OSGAF5 ya Maria Mpale, kuanzia ukurasa wa 6 (Taarifa ya Bunge). Katika taaifa hiyo(anasoma;..)Sehemu hii inaeleza na kukiri namna maoni yaliyopokelewa na Bunge kutoka kwa wadau yalivyosaidia na walalamikaji hawakupinga suala husika
SA Mayunge: Waheshimiwa kwa upande wetu tumetekeleza mambo yote kwa mujibu wa sheria na hata hivyo walalamikaji hawakuzuiwa kutoa maoni. Naomba niende kwenye issue ya 1 ya mahakama kuhusu ratification na kwangu nimebakiza machache tu.
SA Mayunge: Waheshimiwa majaji: Mkataba huu IGA ni Mkataba ya kimataifa unaoweka misingi na maeneo ya ushirikiano hapo baadae. Nirejee katika ibara ya 5(2] ya IGA Kifupi kinasema: kwamba mkataba huu unategemea mikataba mingine ya miradi na huu ulivyo hauwezi kutekelezwa
SA Mayunge: Waheshimiwa majaji IGA kwa hivi ilivyo haivunji kabisa sheria ya Rasilimali Na.6 ya mwaka 2017 kwani IGA sio mkataba wa utekelezaji.
Waheshimiwa majaji vifungu vyote vilivyosemwa na wakili Mwabukusi tunaungana navyo lakini havihusiani na Ratification process.
SA Mayunge: Wahe. Majaji, Irene linus &11 others Vs. TPA &another. Mahakama ya rufaa ilisema sio suala la courtesy bali ni ya lazima. Majaji hawapaswi kutoa maamuzi yanayopingana.Kwa wakati huu mkataba huu upo incapable of violating sheria za Rasilimali, Act no. 5, 6 za 2017
SA Mayunge: Naomba nirejee annexure OSGOF5 Katika ukurasa wa7(Maelezo ya Bunge); kwamba aina ya ubia, kiasi cha ubia kitakuja baadae na sio mkataba huu wa IGA.
SA Mayunge: Na IGA sio mkataba wa mradi wowote wa Bandari na mikataba ijayo ndio inapaswa kutathiminiwa kama inavunja Sheria za Rasilimali, Sura na.5 na sura na. 6 za mwaka 2017
SA Mayunge: Katika uwasilishwaji wa Mwabukusi alirejea mahakama katika Preamble J" ya mkataba wa IGA then ibara ya 2(1) inayoongelea maeneo ya ushirikiano na sisi tunaona is fine kuwa na mawanda hayo.
SA Mayunge: Aliongelea Article 4(2] ya IGA Kama ilikuwa na shida sisi tunaona ipo proper. Yani kutoa taarifa kwa DP World kunashida gani? Anamaliza kwa kuuliza hivyo wakili wa serikali Mayunge.
SA Edwin: Waheshimiwa majaji, kuna malalamiko dhidi ya ibara ya 28 ya katiba. Hii ni ibara inayotoa wajibu kwa watanzania dhidi ya uvamizi wa nchi.
Katika hili lazima kuwa na uthibitisho na lazima ionekane kama kuna vita.
SA Edwin: Na TPA ikiona zinafaaa kwa nchi itaruhusu DP WORLD Kuendelea na uwekezaji na kama itaona haifai haitaruhusu.
Wahe.majaji suala linaloenda kufanyika saizi sio jipya na hata kabla ya DP WORLD Kulikuwa na TICS.
Anasimama wakili wa wananchi senior Mpoki anaweka pingamizi
SA Edwin: Kwa mujibu wa ibara ya 28 ya katiba inasisitiza lazima kuwepo na Vita, na katika mawasilisho ya waleta maombi hatukuonyeshwa kwamba nchi ipo vitani.
Pia hatukuonyeshwa kwamba tumetia Sain kukubali tumeshindwa vita na adui, hatukuonyeshwa na tumeridhia uvamizi ufanyike.
SA Mark: Waheshimiwa yale yote yaliyoombwa na walalamikaji na hata ukichujua katiba yetu na mkataba unakuta hakuna kifungu kilichovunjwa.
Naomba mahakama itamke kwamba kwa mujibu wa taratibu za bunge, wamanchi walipewa muda wa kutoa maoni kwa mujibu wa sheria.
SA Mark: Pia itoe tamko kwamba: mkataba wa IGA ni mkataba wa kimataifa na Serikali yetu ilikuwa na haki ya kuingia katika mkataba husika na haufungwi na sheria zetu za ndani. Taratibu zote za ratification zilifuatwa pamoja na uchambuzi wa kamati ya mkataba wa IGA zilikuwa proper
SA Mark: Na vile vile kwenye mikataba ya aina hii haihitaji consideration.
Kuhusu sheria ya mamunuzi ya Tanzania, mahakama itamke kwamba sheria hii haina nguvu dhidi ya mkataba wa kimataifa (IGA)
SA Mark: Waheshimiwa majaja walalamikaji wameomba maomba takribani 10, tunaomba mahakama itamke wazi kwamba maombi hayapo justified hivyo not granted.
Walalamikaji wameomba maomba takribani 10, tunaomba mahakama itamke wazi kwamba maombi hayapo justified hivyo not granted
SA Mark: Waheshimiwa majaji, katika mazingira kama haya tunaomba kupatiwa gharama zetu na pia shauri hili lifutiliwe mbali (To dismiss the petition with cost to the government)
Naomba kama serikali kuwasilisha
Anamaliza wakili kiongozi wa serikali Bw. Mark.
Adv. Mpoki: Na hichi ndicho kilisemwa katika kesi ya tabora: "Salimu kabora Vs. Tanesco Ltd, ukurasa wa 16" hivyo mahakama kuu haina limited jurisdiction na mnamamlaka ya kuangalia uvunjwaji wa katiba na your defenders of the Constitution.
Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji mna kazi ya kuhakikisha katiba yetu inalindwa na kutovunjwa.
Sasa nije issue ya Constitution: waheshimiwa majaji, wenzetu walitaja ibara ya katiba na sheria na tuna kubaliana nao.
Adv. Mpoki: Lakini kama kweli unataka watu washiriki kuna kanuni kuu tatu [ adequate, sufficient, reasonable) na hakuna hata kimoja kilichotimizwa.
Wanakubali kwamba notice ilitolewa tar 5 June 2023 na kuwataka watu watoe maoni tar 6 June.
Adv. Mpoki: Wanakubali kwamba notice ilitolewa kwa mitandao na wao wanataka tuthibitishe.
Waheshimiwa majaji, the principle is we can't prove the negative but to disprove by evidence.
Kwa mfano nakuambia sina hela halafu unaniambia proof. You can't proof the negative.
Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji tukikubaliana nao tutakuwa tuna water down the essence of notice. Anaweza akaja mtu akatoa notice ya masaa mawili kwenye jambo kama hili?
Angalia walioshiriki ni 72, mmoja peke yake ndio alihudhuria na wengine wote walituma email.
Adv. Mpoki: Wanasema ambaye angefika kutoa maoni angeridishiwa nauli. Lakini tangazo halikutangaza kwamba watao hudhuria watapewa nauli.
Pia wanakubali kwamba waliweka resolution to be adapted lakini hawakuweka mkataba halafu wanaitwa watu kudiacuss mkataba hawapo serious hawa.
Adv. Mpoki anasoma Notice ya bunge ya wito kwa wananchi kutoa maoni ya bandari.
Adv. Mpoki: Nasisitiza kwamba walitaka watu waje kudiscuss azimio la bunge kuhusu mkataba wa bandari ambao wananchi hawaujui.
Adv. Mpoki: Ni rai yetu kwamba notice haikuwa sufficient kwa kuwa watu wameitwa kudiscuss Azimio tar 05.june kabla halijapitishwa na Bunge tar 10.june.
Hii ilipunguza sana ushiriki wa watu waheshimiwa majaji.
Adv. Mpoki: Wenzetu wametoa kesi 2 za South Africa kuonyesha kwamba ni bunge lenyewe linaweza kuamua kuhusu reasonable time.
Kwenye kesi ya kwanza waliyoitumia, wao walipewa siku 30 na walilalamika. Sisi notice ya masaa 24 kulalamika sio jambo baya.
Adv. Mpoki: Na kwamba kitendo chochote cha kutoa notice kusifanye public isishiriki kwa namna yoyote kama hii yetu ilivyokuwa.
Pamoja na kwamba ni bunge lenyewe lina ridhaa ya kuweka notice lakini lengo linapaswa liwe kufanya watu washirki.
Adv. Mpoki: Nimalizie kitu kimoja kwamba, kwa sababu wananchi wamechagua wabunge. Wabunge ni wawakilishi wao. It seems very attractive lakini lakini kifungu cha 108[2] ya kanuni ya Bunge Imewekwa ili wananchi washiriki katika kutoa maoni kwenye mambo yanayowahusu.
Adv. Mpoki: Naomba mahakama hii isichukulie maanani kwamba wabunge wenyewe ndio wanapaswa kushiriki na ndio msingi wa kanunu ya 108[2] ya kanuni ya bunge na haitakiwi kuwa kiini macho.
Adv. Mpoki: Na mwishoni wenzetu katika submission zao wamesema kwa sababu hatukujibu majibu yao hivyo Tumekubaliana. Ni kanuni kwamba mwenzangu akisema mimi nikibisha ndio msingi wa kukutana mahakamani.
Adv. Mpoki: Kwa misingi hiyo hakukuwa na msingi wa sisi kujibu jambo ambalo tushalibishia awali na wao wamejibu na ndio maana tupo hapa.
Waheshimiwa baada ya kusema hayo naishia hapo na namualika msomi Mwabukusi aendelee.
Baada ya wakili Mpoki kumaliza kujibu hoja za mawakili wa serikali, mahakama inaairishwa mpaka asubuhi saa 09:00 ya Tarehe 28Julai 2023 ambapo wakili Boniface Mwabukusi ataendelea kujibu hoja za mawakili wa serikali.
Tukutane kesho asubuhi hapa mahakama kuu Mbeya.
ASANTENI MUNGU AWE NANYI JIONI NJEMA.
Comments
Post a Comment