Posts

Showing posts from May, 2023

KWANINI MADARAKA YA RAIS YANALALAMIKIWA SANA NA NINI KIFANYIKE KWENYE KATIBA IJAYO? MJADALA KATIKA FORUM YA KATIBA YA WATU

Image
  [17:37, 23/05/2023] T Madaraka ya Rais ni mamlaka na nguvu zilizotolewa kwa Rais wa nchi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi husika. Madaraka ya Rais yanajumuisha wajibu wa kusimamia serikali, kutekeleza sera za nchi, na kuongoza shughuli za kiutawala na kisiasa. Kwa ujumla, madaraka ya Rais yanajumuisha mambo yafuatayo: 1.    Uteuzi wa viongozi: Rais anayo mamlaka ya kuteua na kusimamia viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali. Hii inaweza kujumuisha uteuzi wa Mawaziri, wasaidizi wa Rais, majaji, maafisa wa serikali, na wengine. 2.    Utekelezaji wa sheria na sera: Rais ana jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria na sera za nchi. Hii inaweza kujumuisha kusaini sheria, kuongoza na kusimamia shughuli za serikali, na kuhakikisha utekelezaji sahihi wa sera za umma. 3.    Uongozi wa kisiasa: Rais ni kiongozi wa kitaifa na kisiasa wa nchi. Anawakilisha nchi ndani na nje, na ana jukumu la kuweka mwelekeo na maono kwa taifa. Rais anaweza kushiriki katika mikutano ya kimataifa na kuw

RASIMU YA WARIOBA SURA YA KWANZA KWA LUGHA YA ALAMA

Image
       

Kwa ninavyoona watanzania wengi hatuna elimu juu ya sheria na matumizi Bora ya ardhi na mengine mengi yanayohusu Sheria kama ambavyo Mh. Rais alieleza, je ni namna ipi Bora ya kutoa elimu juu ya shiria na matumizi Bora ya ardhi Kwa watanzania

Image
  [22:13, 22/05/2023] +255 6: Nazani njia sahiii ya kutoa elim nikuwatumia maAFSA ardhi kushiriki kwenye mikutano ya vitongoji,mitaa,vijiji,kata,na wilaya kwenye vile vikao vyao na hao waende na kupewa nafasi ili wapate kuifikisha elim na njia sahii ya matumizi bora ya ardhi naomba kuwakilisha [22:15, 22/05/2023] K: @T hoja/swali la @G Linaniletea tafakuri chokonozi kwamba baada ya KATIBA kupitishwa rasmi ni muhimu sana na tena ni HaKI kurudi tena kwa wananchi wa ngazi za vijiji kuwaelimisha juu ya Sheria mbalimbali kama tunataka kuona IMPACT chanya za “ownership of the Constitution” ili pia kudhibiti wale “watukutu” Kwenda na Fedha za mgharibi kuwatumia kwa manufaa yao na waliowatuma   [22:19, 22/05/2023] K: Na hawa maafisa wa ardhi wa Wilaya kama si Kata/Tarafa lazima wawe na checks and balance kwa kuripoti kila kikao na progress na appraisals zao zioneshe ufanisi wake based na productivity ya ardhi uchumi, Kilimo n.k n.k   [22:20, 22/05/2023] M: Sawa kutoa elimu baada ya katiba mp

MDAU KAULIZA Kama haya yote yapo yaani kanuni,sheria na utaratibu tena naona ni kanuni na miongozo kibao..kwanini kuna migogoro ya ardhi tanzania? tatizo ni nini?

Image
    [21:35, 22/05/2023] T: Kuna sababu kadhaa zinazochangia migogoro ya ardhi nchini Tanzania, zikiwa ni pamoja na:   1. Upungufu wa sheria na sera za ardhi: Sheria na sera zisizo wazi, zilizopitwa na wakati, au zisizotekelezwa ipasavyo zinaweza kusababisha migogoro ya ardhi. Mfumo wa kisheria unaweza kukosa miongozo ya kutosha juu ya umiliki wa ardhi, usajili, na matumizi bora ya ardhi.   2. Upungufu wa usimamizi na utekelezaji: Utekelezaji duni wa sheria na sera za ardhi, ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji wa usajili na uamuzi wa migogoro ya ardhi, unaweza kuchochea migogoro kati ya wamiliki wa ardhi na watumiaji wengine.   3. Migogoro ya mipaka: Kutokukamilika kwa mipaka ya ardhi, migogoro ya mipaka kati ya vijiji, wilaya, au mikoa inaweza kusababisha migogoro ya ardhi. Hii inaweza kutokea kutokana na ukosefu wa mipango madhubuti ya upangaji wa ardhi na ucheleweshaji wa mchakato wa kupima na kutambua mipaka rasmi.

MJADALA 22 MEI 2023 KATIKA KATIBA YA TANZANIA,KUNAIBARA ZINAZUNGUMZIA ARDHI KAMA SEKTA KUU AMBAPO HEKTA MRABA MILIONI 44 ZINAFAA KWA KILIMO , HII INAMAANA GANI KATIKA UCHUMI NA RASILIMALI WATU TULIYONAYO? NA WAPI TUMEKWAMA KIKATIBA? TUTOKE VIPI KIKATIBA?"

Image
  [15:17, 22/05/2023] +255 74: Kuna mambo ya msingi katika katiba inayofuata ielekeze kwenye suala la ardhi. 1. Kuhusu umiliki wake uweje...milele, 33, 99yrs? 2. Umiliki wa ardhi ya kijiji upoje? Fidia kwa wananchi kwa ardhi wanazopewa wawekezaji tutumie rates zipi? 3. Nguvu ya rais kama custodian wa ardhi ya nchi inafanywaje iangaliwe kwa upana zaidi? 4. Pia katiba mpya iweke wazi ikiwa rais ataitoa ardhi kwa mwekezaji bila kua na maslahi ya kitaifa yafaa ashitakiwe, na maslahi hayo yawe yenye mashiko! 6. Kuhusu uraia pacha katiba mpya iangalie .....hapa tukiwa wazembe basi ardhi yetu tutaieka rehani kwa wageni wanaotuzunguka wanaotamani ardhi yetu iwe yao. [15:26, 22/05/2023] K: Hizi hoja Kuntu @~ Kwa kuongezea hapa katiba inabidi iweke wazi Ardhi yetu in relation to East Africa na Africa yote maana kuna meulekeo wa mashirikiano ya waafrika lazima tuhifadhi eneo letu ili wageni wasije wakakuta wala   [16:54, 22/05/2023] T: Hili la kilimo NINA MNUKUU MZEE WETU @Mzee K alipata kusema

WANANCHI WA KAWAIDA WANAPASWA KUFANYA NINI JUU YA DIPLOMASIA YA UCHUMI NDANI YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA? MJADALA UNAENDELEA KATIKA FORUM YA KATIBA YA WATU 21MEI 2023 SEHEMU YA KWANZA

Image
  MAJIBU 1 [14:28, 21/05/2023] A: Wananchi wa kawaida wawe na uelewa mzuri juu ya diplomasia ya uchumi kwa kusoma vyanzo vya habari na taarifa za serikali na mashirika ya kibiashara. Pia, wanaweza kushiriki katika mijadala ya umma na kutoa maoni yao juu ya masuala ya uchumi na diplomasia ya uchumi. Kujiunga na vikundi vya mitandao ya kijamii au mashirika ya kiraia yanayohusiana na masuala ya uchumi pia inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi na kushiriki katika shughuli za kijamii. [14:28, 21/05/2023] P\: Hizi sera na sheria zinazotungwa hasa kwenye uchumi wetu... wananchi wa kawaida tunahusishwa kwenye muundo wa sera na sheria?? MAJIBU 2 [14:31, 21/05/2023] b: Katiba ni muhimu kwa sababu ni msingi wa utawala wa nchi na inaongoza jinsi nchi inavyofanya maamuzi yanayohusiana na utawala, sheria, na haki za raia. Katiba pia inaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi, kwa sababu inaweza kuathiri uwekezaji, uchumi wa kibiashara na ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Diplo

SIASA NI UCHUMI KIKATIBA IKOJE? JE, DIPLOMASIA YA UCHUMI KIKATIBA IKOJE? NA MICHAKATO YOTE ILIYOFANYIKA VILIONGELEWA? MJADALA ULIENDELEA TAREHE 20 MEI 2023

Image
   [12:20, 20/05/2023] H: Wadau nawasalimu... Jamhuri ya Tanzania …… Sina budi  kushukuru  viongozi wetu wote kufanya jambo la kihistoria kujenga BOMA,IKULU yetu wenyewe. Nashukuru kwa Kutufungua Macho juu ya Kumbukumbu za Historia ya michakato ya Katiba yetu zinazojadiliwa hapa. Tangu nakuwa ninasikia  hiki kitu..   👉Siasa ni Uchumi,  mara  Siasa za kimataifa  na sasa nina msikia mhe Rais Samia  anasema juu ya Diplomasia ya Uchumi.  Nafikiri ndio hali ya mabadiliko ya sasa kutoka kule Siasa ni Kilimo ya Hayati baba wa Taifa... Wadau mimi naomba tu kujua Siasa ni uchumi kikatiba ikoje? Je, Diplomasia ya uchumi kikatiba ikoje?   Na michakato yote iliyofanyika viliongelewa?  MDAU WA KWANZA AKAJA NA MAJIBU [13:33, 20/05/2023] T:  Siasa na uchumi ni mambo mawili yanayohusiana sana. Serikali na wanasiasa huathiri uchumi kwa kutoa sera, sheria na kanuni zinazosimamia uchumi. Aidha, uchumi pia huathiri siasa kwa sababu hali ya uchumi inaweza kuathiri hali ya kijamii na kisiasa katika nchi hu

SIMULIZI ZA IKULU YA TANZANIA

Image

Opareshani ya +255 imejikita kwenye kuibua changamoto na kuwaeleza Watanzania ni namna gani chama cha CHADEMA kimejipanga kuhakikisha hali za maisha yao inabadilika. Kila kona ya Tanzania wanafika kuongea na wenye nchi.

Image
 

NI LIPI LA KUJIFUNZA JUU YA KUMBUKUMBU YA MUUNDO WA KATIBA YETU NA HISTO...

Image

JE NI LAZIMA KUWEPO NA SHERIA TENA YA KUONGOZA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA? MJADALA ULIENDELEA TAREHE 19 MEI 2023 KWA WAJUMBE KUTOA MAJIBU

Image
[12:33, 19/05/2023] K: Kila BinAdam ana madhaifu na kutegemea na na nani anayasema hayo madhaifu yanaweza kuwa ya kushtusha ila kwa Huyu Ndugu anayeitwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais _Mstaafu _ wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kwa kweli hauwezi kuujadili huu mchakato wa Katiba bila ya kumgusa aghalabu kwa KONGOLE zilizoshiba,  namna ya handling ya mazingira haswa ya kisiasa ilihitaji aina ya busara za kiongozi huyu na Leo tupo Salama kuanza Tena ! Salute 🫡 to this great politician of his time. Tuanze kiduchu hii [13:11, 19/05/2023] T:  Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ambao umeshirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa nchini Tanzania kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba huweza kuchangia mabadiliko makubwa ya kitaifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya Uchumi, Siasa na jamii kwa ujumla.  Mchakato unapokwama pasipo muafaka wa kitaifa huweza kuzalisha mazingira ya kufifia kabisa kwa umoja wa kitaifa na hatimaye kudumaza maendeleo ya nchi.  Na hapa sasa ndio sifa