WANANCHI WA KAWAIDA WANAPASWA KUFANYA NINI JUU YA DIPLOMASIA YA UCHUMI NDANI YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA? MJADALA UNAENDELEA KATIKA FORUM YA KATIBA YA WATU 21MEI 2023 SEHEMU YA KWANZA


 

MAJIBU 1

[14:28, 21/05/2023] A: Wananchi wa kawaida wawe na uelewa mzuri juu ya diplomasia ya uchumi kwa kusoma vyanzo vya habari na taarifa za serikali na mashirika ya kibiashara. Pia, wanaweza kushiriki katika mijadala ya umma na kutoa maoni yao juu ya masuala ya uchumi na diplomasia ya uchumi. Kujiunga na vikundi vya mitandao ya kijamii au mashirika ya kiraia yanayohusiana na masuala ya uchumi pia inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi na kushiriki katika shughuli za kijamii.

[14:28, 21/05/2023] P\: Hizi sera na sheria zinazotungwa hasa kwenye uchumi wetu... wananchi wa kawaida tunahusishwa kwenye muundo wa sera na sheria??

MAJIBU 2

[14:31, 21/05/2023] b: Katiba ni muhimu kwa sababu ni msingi wa utawala wa nchi na inaongoza jinsi nchi inavyofanya maamuzi yanayohusiana na utawala, sheria, na haki za raia. Katiba pia inaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi, kwa sababu inaweza kuathiri uwekezaji, uchumi wa kibiashara na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Diplomasia ya uchumi inahusiana na uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi mbalimbali. Kwa kuzingatia diplomasia ya uchumi, nchi zinaweza kufanya biashara na nchi nyingine, kushirikiana kwenye masuala ya kiuchumi, kushirikiana katika teknolojia na ubunifu, na hata kufanya biashara kati ya nchi na kampuni binafsi. wadau wanaweza nikosoa

[15:18, 21/05/2023]: Diplomasia ya uchumi ni muhimu kwa sababu ina athari kubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Kwa kujenga uhusiano wa kibiashara na nchi nyingine, nchi inaweza kupata fursa za biashara, kuingiza teknolojia mpya na kukuza ajira. Nchi inaweza pia kushirikiana na nchi zingine katika kukuza uchumi wa kikanda na kupunguza umaskini.

[15:23, 21/05/2023] A: Diplomasia ya uchumi pia inaweza kusaidia nchi kujenga uhusiano wa kirafiki na nchi nyingine. Kwa kushirikiana katika masuala ya kiuchumi, nchi inakuwa na fursa ya kuheshimika na kukubalika kimataifa. Hii inaweza kusababisha nchi kupata msimamo mzuri katika masuala mengine ya kimataifa, kama vile siasa, mazingira na haki za binadamu.

[15:24, 21/05/2023] T: Kwa kuongezea, diplomasia ya uchumi inaweza kusaidia nchi kupata teknolojia mpya, mbinu za uzalishaji na mafunzo. Nchi inaweza kushirikiana na nchi nyingine katika kubadilishana uzoefu na teknolojia mpya, na hivyo kusaidia kuongeza uwezo wa uzalishaji wa nchi na kuboresha mifumo ya kibiashara.

Diplomasia ya uchumi pia inaweza kusaidia nchi kushiriki katika masoko ya kimataifa na kupata faida kutokana na biashara ya kimataifa. Kwa kujenga uhusiano wa kibiashara na nchi nyingine, nchi inaweza kufungua masoko mapya kwa bidhaa na huduma za nchi, na hivyo kuongeza fursa za biashara na ukuaji wa uchumi.

[15:25, 21/05/2023] P: Nimesema Wananchi wa Kawaida wanatakiwa haya unayoyasema waelezwe wapewe elimu na kupata ufahamu .Pia kujua hata hao Wawekezaji wanamipaka ya kuwekeza katika Nchi sio kila kitu wanawekeza

[15:27, 21/05/2023] P: Diplomasia ya Uchumi natambua inaweza kukuza Kilimo chetu kwa kubadilisha Elimu na Nchi zingine na hata Masoko.

[15:30, 21/05/2023] P: Unakuta Kiongozi anakuwa Mwenyekiti wa Mtaa ama Kitongoji lakini hajui Wajibu wake kabisa.

Anafanya kikao na kumaliza bila kusema Uchumi wa Mtaa ama Kitongoji upoje kwa muda huo?Miradi ambayo Serikali imeleta ni mingapi na imefikia wapi?kiukweli Elimu ya katiba ni MUHIMU Sana.

[15:31, 21/05/2023] Ta: Ndio maana tumekutana hapa ukisoma malengo kule juu ya kukutana katika forum hii ni kujadili maudhui yatakayosaidia kumfikia na kuelewa bila kulishwa maneno wala kuambiwa uongo juu ya upatikanaji wa katiba bora..Tukakubaliana tuanze kwanza na Kumbu kumbu ya muundo wa katiba yetu tangu ukoloni..tuje na hii ya sasa,mapungufu na mazuri,tuvuke nayo twende rasimu ya Warioba tudadavueee Turudi ile pendekezwa...kwa wakati huu wote tunachokijadili hapa kinachakatwa na kuwajuza wananchi wenzetu kwa lugha nyepesi inayoeleweka...LINA WEZEKANA NA NDIO TUMEANZA kwa sasa tunajadili muundo na kumbukumbu

[15:53, 21/05/2023] M: Nini wajibu wa Viongozi sasa kwenye hiyo diplomasia ya uchumi hapa Tanzania maana ukiangalia hizi balozi za wenzetu wako bize mno miradi ya kufa mtu wanaiibua ndani ya nchi kuna taasisi kibao na nyingine hata zinakiuka utendaji wao na katiba yenyewe?

[15:56, 21/05/2023]pa: Ni kweli kabisa hili wengi hawajui

MAJIBU 4

[15:59, 21/05/2023] A: wajibu wa viongozi katika diplomasia ya uchumi Tanzania ni kuhakikisha kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na mataifa mengine unaendelea kuimarika. Inahitaji juhudi za pamoja za viongozi kufanya kazi na kushirikiana ili kuhakikisha kwamba mahusiano kati ya nchi na wengine yanakuwa bora zaidi. Viongozi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa diplomasia ya uchumi inaleta faida katika kujenga uchumi na maendeleo ya Tanzania.

[16:20, 21/05/2023] A: Kwa mfano, viongozi wa Tanzania wanaweza kushirikiana na wenzao wa mataifa mengine kama anavyofanya Rais wetu Dr.Samia Suluhu Hassan, katika kukuza biashara na uwekezaji. Pia tunaona akishirikiana nao katika kuboresha elimu, afya, miundombinu na teknolojia. Viongozi wanaweza kuwa mstari wa mbele katika kukuza utalii kati ya Tanzania na mataifa mengine si tumeiona Loyal tour, na kuongeza ushirikiano wa kitamaduni kati ya watu wa nchi na nchi. Kwa ujumla, viongozi wanapaswa kufanya kazi pamoja na kuunga mkono juhudi zote za kiongozi wa nchi ili kuhakikisha kuwa diplomasia ya uchumi inaleta manufaa kwa wananchi wa Tanzania kwa ujumla wake.


[16:51, 21/05/2023] M: Kwa maoni yangu, sijaona watu kuchangia kwenye mjadala huu, ni vifungu gani vinahitaji kupewa kipaumbele katika mchakato huu wa Katiba. Aidha pia sijaona pendekezo lolote kutolewa juu ya jinsi ya kuukwamua mchakato ili kusonga mbele. 

Kama sisi wenyewe humu hatusemi hiki wala kile, bali tukisisitiza tu kwamba wananchi washirikishwe zaidi kwenye kazi hii iliyopo mbele yetu, lakini sisi wenyewe hatusema nini cha kubadili, kuongeza au kusahihisha, mwananchi wa kawaida ataweza kweli! Nilisema hapo awali, suala la Katiba, ni la kitaalamu zaidi. Hivyo kwa mtazamo wangu, tusubiri kuona wale watakaoshiriki kwa ujumla wao, watakuja na mapendekezo gani juu ya kusonga mbele kupata Katiba hiyo tunayoitarajia.

[17:19, 21/05/2023] P: Ni kweli

[17:37, 21/05/2023]P: Nafikiri sisi ni wananchi pia...tuna haki na wajibu wa kuchangia ndio maana tuko humu....

MAJIBU 5

[17:49, 21/05/2023] K: Naomba niongezee kidogo diplomasia ya uchumi ina jukumu muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya watu. Kwa mfano, kupitia diplomasia ya uchumi, nchi inaweza kushawishi nchi nyingine kuwekeza katika sekta za maendeleo, kama vile afya, elimu, miundombinu, na kilimo.

Diplomasia ya uchumi pia inaweza kusaidia nchi kupata fursa za biashara na uwekezaji. Kwa kuwa na uhusiano wa karibu na nchi nyingine, nchi inaweza kushawishi nchi hizo kuwekeza katika sekta za kiuchumi za nchi yao. Hii inaweza kusababisha kuundwa kwa ajira na kuongezeka kwa mapato ya nchi.

[17:51, 21/05/2023] P: Hili swali sijashibishwa majibu...

[17:57, 21/05/2023] P: Tunajadili diplomasia ya uchumi ila mimi mwananchi wa kawaida nawajibika vipi kwenye hii diplomasia ya uchumi? Na diplomasia hii ya uchumi itanilindaje kwenye katiba ijayo... naomba nisaidiwe kutafakari tupate majibu.

[18:02, 21/05/2023] K: Labda niweke hivi pia kwa mtihani wa Loval Government na Uhusiano wa Kidiplomasia ; Kwa mfano, viongozi wa Kata Fulani au Wilaya Fulani  wanaweza kushirikiana na wenzao wa Kata au Wilaya nyingine kama anavyofanya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Ngazi ya Kitaifa, kwenye eneo la kukuza biashara na uwekezaji wa kata au Wilaya husika.  Pia Viongozi hawa wanaweza kushirikiana na Viongozi wenzao wa Serikali za Mitaa katika kuboresha elimu, afya, miundombinu na teknolojia. Viongozi haw haw wa Kata ama Wilaya wanaweza wakiwa mstari wa mbele katika kukuza utalii wa ndani ya Tanzania na mataifa mengine (kwa maana ya kwamba  wageni wakija watapitavSerikalibya Mitaa. Kwa ujumla, viongozi _wanapaswa _ kufanya kazi pamoja na kuunga mkono juhudi zote za kiongozi wa nchi ili kuhakikisha kuwa diplomasia ya uchumi inaleta manufaa kwa wananchi wa Tanzania pia kwenye Vijiji vyetu. 

#think globalactlocal


[18:04, 21/05/2023] T: Uchumi wa kikatiba ni aina ya uchumi ambao serikali inashiriki kikamilifu katika kusimamia na kusimamia rasilimali za nchi. Kwa hivyo, sheria zinazohusiana na uchumi wa kikatiba mara nyingi huainisha jinsi serikali inavyodhibiti na kusimamia rasilimali za nchi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi.

[18:11, 21/05/2023] K: Sawa kabisa, Katiba huwa unatudai Muongozo tu wa namna ya kufanya kwa ujumla wake katika neo fulani katika “muktadha” wa utekelezaji wa Sera na utungwaji wake. 

Kwa hiyo katiba ikitoa Muongozo Bunge hunting’s Sheria ya utekelezaji wa Jambo ambalo mamlaka husika na wananchi wameridhia lifanyike.

Na kwa kuwa Bunge ni “baraza la kutunga sheria lenye uwakilishi wa watu wa kila eneo la nchi” hivyo basi Sheria ikitungwa ni wananchi wametunga kwa kuwakilishwa.

Asanteni.

[18:12, 21/05/2023] T: Kwanza tulisema baada ya kuuangalia muundo na Historia yake tutakuja kuangalia mapungufu na nni wenzetu 2012-2015 walikiona katika katiba ya 1977..na mapendekezo yao katika Rasimu ya Warioba..ukirudi huku mtaani kunajadiliwa mengi mno yanayohusu Katiba na kubwa si kuijua hapana kubwa ni kuipata nyingine...sasa Tuijue na ndio maana hapa kuna maswali na majibu hadi tunafikia muafaka..ukiangalia vilili majukwaa kuna kampeni kubwa inaendeshwa..Hapa kuna wataalamu wote wa Siasa,katiba na uchumi..na kubwa ni namna bora tutaelewa yaliyomo na yajayo...


MJADALA UNAENDELEA...

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya utawala wa Kijerumani katika eneo la Tanganyika inahusisha kipindi cha ukoloni wa Kijerumani ambacho kilidumu kati ya mwaka 1885 na 1916

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 23 OKTOBA, 2022