JE NI LAZIMA KUWEPO NA SHERIA TENA YA KUONGOZA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA? MJADALA ULIENDELEA TAREHE 19 MEI 2023 KWA WAJUMBE KUTOA MAJIBU
[12:33, 19/05/2023] K: Kila BinAdam ana madhaifu na kutegemea na na nani anayasema hayo madhaifu yanaweza kuwa ya kushtusha ila kwa Huyu Ndugu anayeitwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais _Mstaafu _ wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kwa kweli hauwezi kuujadili huu mchakato wa Katiba bila ya kumgusa aghalabu kwa KONGOLE zilizoshiba, namna ya handling ya mazingira haswa ya kisiasa ilihitaji aina ya busara za kiongozi huyu na Leo tupo Salama kuanza Tena ! Salute 🫡 to this great politician of his time.
Tuanze kiduchu hii
[13:11, 19/05/2023] T:
Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ambao umeshirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa nchini Tanzania kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba huweza kuchangia mabadiliko makubwa ya kitaifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya Uchumi, Siasa na jamii kwa ujumla.
Mchakato unapokwama pasipo muafaka wa kitaifa huweza kuzalisha mazingira ya kufifia kabisa kwa umoja wa kitaifa na hatimaye kudumaza maendeleo ya nchi.
Na hapa sasa ndio sifa zangu zinamwangukia Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan,anayaona haya kwa mapana sana..
Swala la Maridhiano na kuanza upya ni Maono ya juu mno ya Dr Samia binafsi...
Tanzania iliamua kuanza uandishi wa katiba mpya kutokana na kua katiba zote tano zilizopita tangu katiba ya uhuru ya mwaka 1961 mpaka katiba ya kudumu ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake yote 14 vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutoshirikisha wananchi kikamilifu.
Hivyo ukaundwa mfumo ambao ungeruhusu ushiriki wa wananchi katika kupata katiba bora.
Pamoja na kukwama kwa kwa mchakato wa mabadiliko ya katiba mnamo mwezi Aprili 2015 ambao ulianzishwa mnamo mwaka 2011,
Ukifuatilia hotuba nyingi za Dr Samia ambae alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la katiba wakati huo anataka wananchi waelewe wafafanuliwe watambue mambo mawili tu
MOJA
Sababu kuu za kukwama kwa mchakato wa katiba;
PILI
Mapendekezo ya njia nzuri za kuufufua na kuendeleza mchakato wa Katiba ambao unabeba maoni ya wananchi.
Na hata ukiyasoma matakwa ya wanaharakati na asasi za kiraia utakuta wanaunga mkono hili hiki ndio wadau wengi hapa wamesisitiza tukianishe...
[13:15, 19/05/2023] T:
Tarahe 31 Disemba 2010 aliyekuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza nia ya Serikali ya kuanzisha mchakato wa Katiba. Hatimaye mwaka 2011 Mchakato huo ulianza kwa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 na baadaye kufuatiwa na Sheria nyingine ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitamka kuanzishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo iliratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya katiba ambayo pia ilihaririwa na Mabaraza ya Katiba na hatimaye kupatikana kwa Rasimu ya Pili ya Katiba. Rasimu hiyo
iliwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba (BMK) ambalo kwa kiasi kikubwa lilitawaliwa na wanasiasa wakitokana na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar.
Mchakato wa Bunge Maalum kujadili na kutunga Katiba Inayopendekezwa kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na mivutano ya kisiasa na kusababisha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujitoa kwenye majadiliano na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Kujitoa kwa wajumbe
hawa kulisababisha kutungwa kwa Katiba Inayopendekezwa iliokosa muafaka na kuidhinishwa Mwezi Oktoba 2014.
Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11/2013, Tume ya Uchaguzi ilipanga tarehe 30 Aprili 2015 kuwa ndiyo siku ya wananchi kupiga kura yamaoni. Zoezi la kura ya maoni lilikwama kufanyika kwa sababu mbalimbali....KONGOLE SANA DR JAKAYA KIKWETE
[13:27, 19/05/2023] T:
SABABU ZA KUKWAMA KWA MCHAKATO WA KATIBA ZILITAJWA TAJWA MARA KADHAA
Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni na Maelekezo ya Tume ya Uchaguzi (NEC), zoezi la kura ya maoni lilipangwa kufanyika tarehe 30 Aprili 2015. Lakini kutokana na sababu mbalimbali zoezi la kupiga kura ya maoni lilishindikana na kuahirishwa kwa kipindi kisichofahamika.
Sababu mbalimbali zilizopelekea kuahirishwa kwa zoezi la upigaji wa kura yamaoni juu ya Katiba Inayopendekezwa ni pamoja na;
i. Kutengwa kwa muda finyu na usio halisi wa kisheria kutekeleza zoezi la Upigaji kura ya Maoni. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura yaMaoni, Rais aliiagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa kura ya maoni kufanyika tarehe 30 Aprili 2015, lakini wakati huo huo Tume ya Uchaguzi ilikua ikiendesha programu ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa njia ya kielektroniki ili kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kinyume na ilivyokua imepangwa, zoezi la kuboresha daftari lilichelewa kumalizika kwa muda muafaka, hivyo kupelekea muda kuwa finyu na hatimaye tarehe za kura ya maoni zilizopangwa kisheria kupitwa na wakati.
ii. Sababu nyingine ni kutokuwepo kwa muafaka wa kikatiba ndani ya Bunge Maalum la Katiba na hivyo kupelekea baadhi ya wajumbe wa BMK hususan waliotokana na Vyama vya Upinzani - Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kijitoa na kutoshiriki katika kuipitisha
Katiba Inayopendekezwa na kuchangia kujitokeza kwa mgawanyiko mkubwa katika jamii na kuathiri mwenendo mzima wa mchakato wa katiba.
Kwa kiasi kikubwa mpasuko wa BMK ulichangiwa na uwepo wa idadi kubwa ya wanasiasa ambao waliteuliwa kuwa wajumbe huku wakiwa bado ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar.
Lakini nakumbuka wakati ule kamati iliyokuwa ikiongozwa na Dr Khoti Kamanga ilichambua kwa kina kukwama kwa mchakato mzima..Twendeleeeeee
[13:28, 19/05/2023] P: Said it all well. ACTION!
[13:47, 19/05/2023] T: NAKUNUKUU @Pasta Martin
"Chimbuko la mamlaka ya dola ni wananchi wenyewe. Serikali hupata uhalali wake kutokana na wananchi kupitia Katiba. Vilevile kushiriki kwa wananchi katika maamuzi kuhusu mambo yanayogusa maslahi yao ni msingi mkuu wa utawala wa ki-demokrasia. Kwa misingi hiyo,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko katika mchakato wa kupata Katiba mpya. Kwa kuwa Katiba ni uamuzi wa wananchi jinsi wanavyotaka kuishi, kujiongoza na kuendesha nchi yao,
mabadiliko ya Katiba yanawapatia Watanzania fursa kubwa ya kuzaliwa upya kikatiba, kisheria, kisiasa, kiuchumi na kijamii".-@Pasta Martin akihojiwa rfikiswahili 2011 hayo ya mbele uliyoyasema wakati ule utaya ongezea mwenyewe...Media haifichagi kitu
[13:52, 19/05/2023] A: Kutoka Maktaba! 😀💪🏽
[13:52, 19/05/2023] T: Na maneno haya yalitumika katika utangulizi wa mwongozo wa ELIMU KUHUSU KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA YA MWAKA 1977
(KWA LUGHA NYEPESI) uliotolewa na TUME YA MABADILIKO YA KATIBA wakati huo Kudos @Pasta Martin
[13:53, 19/05/2023] K: Teknolojia ni ya kuheshimu
[14:07, 19/05/2023] Ta:
SHERIA ZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA
Kuna sheria kuu mbili zilizoongoza mchakato wa mabadiliko ya katiba ambazo ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83 ya mwaka 2011 pamoja na Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11 ya mwaka 2013.
Sheria ya Mabadiliko ya katiba ilitoa muongozo wa kuundwa na mamlaka ya vyombo vyote vya kuratibu mchakato wa katiba, vikiwemo; Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba.
Sharia hizi pia zimeainisha namna ya ushiriki wa wananchi katika hatua zote za mchakato wa katiba, utaratibu wa wananchi kuipigia kura ya Maoni Katiba Inayopendekezwa pamoja na vyombo vitakavyosimamia haswa Tume ya Taifa Uchaguzi. Kwa kiasi kikubwa hatua zote za mchakato zinazotamkwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba zimekwisha kamilika. Kwa upande wa Sheria ya Kura Maoni, hatua pekee ambayo haijakamilika mpaka sasa ni kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa kupitia kura ya maoni na kuanza kutumika rasmi.
Wakati wa kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni, ilizaniwa kuwa mchakato wa katiba utakamilika ndani ya muda uliokuwa umekusudiwa kisheria.
Kwa bahati mbaya muda ulikwisha kabla ya Katiba Inayopendekezwa kupigiwa kura ya maoni kutokana na sababu mbalimbali zilizoanishwa awali, ikiwemo uwepo wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa njia ya kielektroniki kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kutokana na kupita kwa muda kisheria, maboresho ya Sheria ya Kura ya Maoni hayaepukiki ili kuruhusu mwendelezo mzima wa mchakato wa kupata katiba mpya. Ref. MCHAKATO WA KATIBA MPYA NINI MWISHO WAKE? Lhrc -2018
MJADALA UNAENDELEA
Comments
Post a Comment