MKUTANO WA KAMATI YA UONGOZI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA JULAI 31, 2023,

 

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa mara baada ya kumaliza kikao cha kamati hiyo  jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Annamringi Macha, Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Juma Khatib na kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mzee John Momose Cheyo. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. (Picha na ORPP)


Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vya Siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Momose Cheyo akichangia mada wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.


Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vya Siasa, Bibi. Dorothy Semu (kulia) na Rashidi Rai wakipitia taarifa wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.



Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vya Siasa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT - Wazalendo, Bibi. Dorothy Semu akichangia mada wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika kesho tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.




Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha kamati hiyo  tarehe 31 Julai 2023 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.


Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa ufunzi wa kikao hicho  tarehe 31 Julai 2023 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Uhusiano wa Umma, Bw. Doyo Hassan Doyo, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Annamringi Macha na Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Juma Khatib. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika  tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog

Historia ya utawala wa Kijerumani katika eneo la Tanganyika inahusisha kipindi cha ukoloni wa Kijerumani ambacho kilidumu kati ya mwaka 1885 na 1916

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 23 OKTOBA, 2022