MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA TATU

TAREHE 27 JULAI 2023 MAJAJI WANAINGIA MUDA  SAA 09: 44 ASUBUHI.

MAJAJI WATATU;

1. Hon. Ndunguru

2. Hon. Ismail

3. Hon. Kagomba

Wote wameinama wanaandika

Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.

MAWAKILI WA SERIKALI;

1. Adv. Mark Muluambo

2. Edson Mwaiyunge

3. Alice Mkulu 

4. Stanley Kalokola

5. Edwin Lwebilo.

MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI;

1. Mpale Mpoki

2. Boniface MWABUKUSI 

3. Philip Mwakilima 

4. Livino Ngalimitumba.

Anasimama wakili kiongozi wa serikali Mr. Mark na kuijulisha mahakama kuwa wako tayari kuendelea na majibu yao.

Mahakama inaruhusu.

SA Kalokola: waheshimiwa naendelea na hoja namba 6 kama mkataba huu IGA ulizingatia sheria ya Manunuzi (Procurement Act)

SA Kalokola: Hoja hii inatokana na ombi na 4 ya Origjnating summons kwamba IGA haikuzingatia Sheria ya Manunuzi.

Na katika aya ya 12, walalamikaji wanasema kuna tender inetolewa kwa DP WORLD Kinyume na sheria za manunuzi.

SA Kalokola: Majibu yetu yapo katika aya ya 14 ya kiapo cha  Mohamed Salumu kwamba; Hakuna tender iliyotolewa na hakuna majibu yaliyoletwa na wenzetu kupinga hili.

Waheshimiwa majaji wenzetu waliandika jina la kampuni DPW na sisi tunajua kuwa kuna kampuni ya DPW Na hawakukanusha

SA Kalokola: Pia kwa Kuwa Mkataba wa  IGA ni mkataba wa Kimataifa unasinamiwa na sheria za kimataifa hivyo sheria ya manunuzi haiwezi kutumika bali sheria za kimataifa.

SA Kalokola: Waheshimiwa Mkataba huu ni framework agreement ni mkataba wa ushirikiano  wenye mifumo ya uwekezaji kitu ambacho hakiwezi kuhusiana na dhana ya manunuzi kana kwamba kuna nchi inamnunua mwengine.

Hivyo wenzetu hawakupaswa kulazimika kuja na hoja ya kimanunuzi.

SA Kalokola: Wakili Mwakilima alisema kuhusu sheria ya manunuzi naomba tuongozwe  na kifungu cha 12 cha Tanzania Port Act. Kunachozungumzia Kazi za TPA.

Majukumu ya TPA ni kupromote local &FOREIGN  investment kwenye bandari. Na kama wenzetu wangeanzia katika dhana ya uwekezaji.

SA Kalokola: Kunapokuwa na International obligations  na inakinzana na sheria za ndani, Sheria za kimataifa zitasimama dhidi ya sheria za ndani hivyo masharti yaliyopo kwenye IGA yanasimama.

SA Kalokola: Na kwamba Mkataba wa IGA haukuzingatia matakwa ya sheria ya manunuzi is a misconception (Kupotoka).

Yaani wametumia dhana fulani kwenye eneo ambalo sio mahala pake. Hivyo hoja ya 4 na 5 na 6 kwenye matumizi ya mikataba nimejibu hivyo na naomba hoja zangu zizingatiwe

SA Kalokola: Waheshimiwa majaji Walalamikaji wameshindwa kuthibitisha hoja zote tatu na niombe mahakama irejee kwa shauri la Center for strategic litigation Ltd & another Vs. AG and others.

Anamaliza wakili wa serikali Bw. Kalokola sasa anamkaribisha wakili mwingine wa serikali kuendelea kujibu.

Anafuata wakili wa serikali aitwaye Mayunge.

Sasa ni zamu ya wakili wa serikali aitwaye Mr. Mayunge na ni wakili wa tatu wa serikali katika kuwasilisha majibu kwenye kesi hii ya bandari.

SA Mayunge: amekaribishwa na anaendelea. Nitaanza kujibu hoja namba 2 ya Senior Mpoki:

SA Mayunge: Waheshimiwa, Nikirejea ibara ya 21(1] ya Katiba ya Tz, kimsingi inaelezea kuchagua na kuchaguliwa kwa wabunge na kwamba ni wawakilishi wa wananchi.

Pia ibara ya 63(2] ya Katiba ya Tz, maudhui yake ni kwamba Bunge linasimama kwa niaba ya wananchi kuisimamia serikali

SA Kalokola: Nirejee pia ibara ya 63(3]e ya Katiba Tanzania inayotamka kwamba; utekelezaji wa madaraka ya  Bunge: ni kujadili na kuridhia mikataba.

Nirejee 89(1],(2] ya Katiba ya Tanzania, inayosema bunge litatunga kanuni za kudumu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake.

SA Mayunge: Ibara ndogo ya [2) Bunge kutunga kanuni ndogo za utekelezaji lakini pia ibara ya 96inayoeleza: BUNGE Laweza kuunda kamati mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza madaraka ya Bunge.

SA Mayunge: Waheshimiwa, kutokana na ibara ya 89(1] Bunge la JMT limetunga kanuni za kudumu kama ilivyoelekezwa mfano kanuni ya 108 ambayo nitasoma kanuni ndogo ya 2.(Quote as its )

SA Mayunge: Waheshimiwa katika kiapo cha Maria ambacho pia ni kiapo cha Bwana Salum, serikali iliwasisha Mkataba wa IGA bungeni kwa ajili ya ratification.

Katika aya ya tatu anaeleza jinsi serikali ilivyopeleka mkataba Bungeni kupitia barua iliyoambatanishwa.

SA Mayunge: Pamoja na yote yaliyoandikwa naomba nisome aya ya kwanza: Baada ya kukamilika shughuli za serikali, Kutokana na umuhimu wake tunaomba kuwasilisha shuguli 7 ili Bunge lifanyie kazi kwa mambo yafuatayo.

SA Mayunge: 1. Kuazimia azimio la serikali kuingia Mkataba wa IGA na DP WORLD From Dubai. Baada ya hapo kanuni ya 108[2] ikaanza kutekelezwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na bunge.

SA Mayunge: Na bunge ilialika wadau ili watoe maoni yao kupitia Notice iliyoambatanishwa kwenye kiapo cha Maria, kiambata OSGF2 Kwenye aya ya 5.

Wahe. majaji naomba nisome kiapo husika ili muone kama it was reasonable

Majaji : wanamruhusu

Wakili: Serikali: anasoma barua husika

SA Mayunge: Kwa ujumla notice inahusu Mkutano wa Kupokea Maoni dhidi ya mkataba wa IGA.

Waheshimiwa majaji, hili tangazo waliliona waleta maombi na niwao wameeleza katka kiapo chao, aya ya 11 walivyopata tangazo hilo.

SA Mayunge: Na katika kiapo chao hawajasema muda ulikuwa mfupi sio kwamba uliwazuia kutoa maoni na hawajasema chochote.

Na hatujua walalamikaji wanalalamika kwa niaba ya nani na hwapo hapa kwa niaba ya nani.

SA Mayunge: Waheshimiwa majaji wenyemaoni walikuepo japo hawakuwa wao na ndio maana waheshimiwa majaji katika aya ya 7 ya kiapo cha Maria kimesema watu 72 walitoa maoni.

SA Mayunge: Wale waliokuwa wanataka na wakatoa maoni, sasa haya maombi haya ni just speculations, na hata hawakushiriki kutoa maoni lakini wanalalamika.

Na hakuna hata malalamiko ya barua ya kuomba kuongezewa muda wa kukusanya maoni.

Jaji: kwahiyo unasema muda ulikuwa reasonable?

SA Mayung:  it was duly saved, adequate and reasonable na waheshimiwa sasa ni wakati wa utandawazi mtu anaweza kutoa maoni yake popote kuputa barua pepe.

SA Mayunga: Waheshimiwa waliotoa maoni walitoka Mwanza, Arusha, na sehemu mbalimbali za nchi wote hao walitoa maoni yao.

Katika kanuni ya 108(2] ya Kanuni ya Bunge haikutoa kabisa suala la muda na kunasababu zake nitafafanua.

SA Mayunge: Waheshimiwa kwanin tuna tunasema muda ulitosha: ni Bunge lililohitaji maoni kutoka kwa watu.

BUSARA YA BUNGE; Bunge kwa busara zao waliona muda waliotoa unatosha kwa watu kutoa maoni yao dhidi ya Mkataba wa IGA.

SA Mayunge: WAHESHIMIWA suala la reasonable linategemea mazingira, umuhimu, uharaka na mengine mengi ngoja nitaje kidogo.

Suala la Reasonableness kwa masuala ya Bunge, mahakama kadhaa kutoka sehemu mbalimbali duniani zimejadili suala hili na tusiwe tofauti na mahakama zingine.

SA Mayunge: Naomba turejee Uamuzi wa Africa kusini Doctor for life .V. Speaker of National Assembly &Others katika ukurasa wa 70, paragraph  2.

Mahakama ilisema: reasonableness is.....(anasoma) kimsingi reasonableness  inategemeana na mambo kadhaa.

SA Mayunge: Kwamba mahakama haiwezi kuipangia bunge. Kwamba Bunge ndio lilihitaji maoni na ndio linalojua kiwango cha ushirikishwaji wa wananchi na vile vile mahakama haitegemei kulibishia Bunge kuhusu reasonableness

SA Mayunge: Waheshimiwa  hivyo masuala ya kutaka miezi sijui 6 kwa ajili ya maoni hiyo ni busara ya Bunge na si vinginevyo.

Jaji: Nani kasema miezi 6

Wadau: wanacheka 😂

Adv. Mpoki: Hizo ni imagination  zake Waheshimiwa  majaji.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya utawala wa Kijerumani katika eneo la Tanganyika inahusisha kipindi cha ukoloni wa Kijerumani ambacho kilidumu kati ya mwaka 1885 na 1916

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 23 OKTOBA, 2022