HISTORIA YA KUTUNGA KATIBA NA USHIRIKI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA
Historia ya chama cha siasa kuchukua jukumu kuu katika mchakato wa kutunga katiba (au hata kufanya marekebisho ya vifungu/vipengele vyake) unaweza kujadiliwa kuanzia mwaka 1961.
Ikumbukwe kuwa Tanganyika (sasa Tanzania) ilijipatia Uhuru wake mwaka huo toka kwa wakoloni wa Kiingereza kwa njia ya katiba iliyoruhusu “demokrasia” ya uwakilishi wa vyama. Hivyo baada ya chaguzi za kabla ya Uhuru, ni chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ndichokilishinda viti vyote na kushika dola.
Katiba hiyo iliruhusu pia vyama vya kiraia kama vile vyama vya wafanyakazi, wanawake, na vijana kufanya shughuli zao. Lakini kutokana na lile lengo kuu la chama cha siasa kushika dola, TANU ilianza kujipanga na kuhodhi madaraka ya nchi hususani kwa kuanzisha sheria mpya.
TANU ilianza mradi mkubwa wa kutunga katiba mpya.Hapo Tanzania ikajikuta ikitunga katiba mpya kama nne:
Katiba ya Jamhuri (1962), Katiba ya Muungano (1964), Katiba ya Chama Kimoja (1965) na Katiba ya Kudumu (1977).
Comments
Post a Comment