HISTORIA FUPI YA MUUNDO WA KATIBA WAKATI WA WAKOLONI HADI SASA
Ilitufikie malengo ya kutambua na kuelewa kwanini Katiba ni muhimu katika Nchi, yapaswa tujue Historia Pana ya Katiba na Sheria zeta kabla na baada ya Ukoloni fuatana nasi Hapa kutambua Katiba ya Watu ni ipi hasa
Kwa ujumla nchi nyingi hasa zile zinazoendelea zina katiba zilizoandikwa.nyingi kati ya katiba hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka.Katiba hizo ni maridhiano ambayo yalilinda maslahi ya pande zote mbili:
(1)Tawala za kikoloni zilizokuwa zikiandika.
(2)Nchi iliyokuwa ikipata uhuru
"Katiba nyingi katika nchi zilizoendelea zina uhusiano na Katiba na Tawala
za kikoloni.
Historia ya katiba hapa Tanzania pia ina uhusiano na tawala za kikoloni
zilizokuwa zinatawala kabla ya uhuru
Historia Ya Mabadiliko Ya Katiba Tanzania 1961 Katiba ya kwanza ya uhuru iliyowekwa na Waingereza (Independence Constitution).
Mwaka 1962 Katiba ya Jamhuri (The Republic Constitution) iliitambua Tanganyika kama Jamhuri na ilipunguza madaraka ya Bunge(Iliwekwa na Waingereza).
Katiba Hiyo iliruhusu mfumo wa vyama vingi, na Vyama vifuatavyo vilisajiliwa:TANU, United Tanganyika Party(UTP), African National Congress(ANC), The Peoples Democratic Party(PDP), Peoples Convertion Party(PNP), National Enterprise Party(NEP), All Muslim Nationalist Union of Tanganyika(AMNUT), African Independence Movement(AIM).
Lakini mwaka 1963 Halmashauri Kuu ya TANU ilipitisha maamuzi kufanya Tanganyika kuwa nchi ya chama kimoja.Ikafuatia mwaka 1965 Sheria ya chama kimoja iliingizwa kwenye Katiba
Mwaka 1965 Iliwekwa katiba ya muda (The Interim Constitution)
Mwaka 1977 Haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika Dibaji.Mwaka 1984 Katika katiba ya Jamhuri haki za binadamu ziliingizwa rasmi katika katiba.Mwaka1992 Katiba iliruhusu tena mfumo wa vyama vingi kwa shinikizo la nchi za kibeberu
Comments
Post a Comment