MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI, UKIJADILI NA KUPOKEA MAONI YA MSWADA WA SHERIA ZA UCHAGUZI NA SHERIA ZA VYAMA VYA SIASA. Baraza la Vyama vya Siasa nchini liliandaa Mkutano Maalum wa kujadili na kupokea maoni ya Wadau juu ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa ambayo ni matokeo ya mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mgeni Rasmi katika mkutano huu alikuwa Bw. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wadau na Washiriki walijulishwa na kuhusu lengo la Mkutano, pamoja na mambo mengine, ilielezwa kuwa ni Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaojadili na kupokea maoni ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa Kauli mbiu ya mkutano huu Ilikuwa ni “ Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia ”. Mara baada ya maelezo haya. Mkutano huu uliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera...
Popular posts from this blog
MKUTANO HUU UMEKUWA WENYE TIJA KWANI MMETOA MAONI KWA KUZINGATIA MASLAHI MAKUBWA YA NCHI YETU - MHE. DOTO BITEKO Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaungana na watu wengine waliosema hapa nami nitoe shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa Juhudi zake ameweza kuimarisha ustawi wa Demokrasia hapa nchini sambamba na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuwaletea maendeleo Watanzania" "Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amekuwa mfano wa kuigwa kitaifa na kimataifa kuhakikisha Demokrasia yetu inazidi kustawi na kuifanya Demokrasia yetu kuendeshwa kwa misingi ya haki, utawala bora na kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea na bila kusahau mazingira ya watu ambao bila wao Serikali haipati uhalali" "Mkutano huu umekuwa wenye tija na mimi nimekuwa nikiufuatilia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mmezungumza mengi kutokana na Ajenda mlizomuwa nazo na ni wazi kabisa wadau waliokuwa wengi wametoa maon...
MJADALA [14:55, 20/01/2024] +255 769: Tudai katiba mpya ITAKAYO wafanya watawala wa wajibike kwa wananchi MAJIBU [00:51, 21/01/2024] T: Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba mafanikio ya uwajibikaji wa serikali na viongozi yanaweza kutegemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na muundo wa katiba na utekelezaji wake. Ni kweli Katiba inaweza kuwa msingi wa kuanzisha mfumo wa uwajibikaji. Inaweza kuainisha madaraka na majukumu ya viongozi, kuhakikisha uwazi wa shughuli za serikali, na kutoa njia za kudhibiti mamlaka. Hata hivyo, hata katiba nzuri inaweza kushindwa kufikia lengo lake ikiwa hakutakuwa na utendaji mzuri wa taasisi za serikali, uwajibikaji wa kijamii, na mfumo mzuri wa kisheria. Ibara inayohusu uwajibikaji katika Katiba ya Tanzania inaweza kuwa Ibara 9. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kwamba mafanikio ya uwajibikaji hayategemei tu kwenye kifungu hicho bali pia utekelezaji wake katika mazoezi ya kila siku. Kwa kuzingatia haya, ikiwa kuna mapungufu katika uwajibikaji, ni muhimu kutathmin...
Comments
Post a Comment