WAZIRI NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA KITUO JUMUISHI



Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Khatibu Kazungu akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022. 


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza  Novemba 29, 2022. 

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Patience Ntwina.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro amepongeza jitihada hizo na ushirikiano uliooneshwa kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa  kufanikisha ndoto hiyo ya kuwa na Kituo Jumuishi.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa ujenzi huo utawezesha kupunguza na kuondoa gharama kwa wateja kwa kuwa utawawezesha kupata huduma sehemu moja.

Comments

Popular posts from this blog

UTARATIBU WA USAFI WA MAZINGIRA NAO UWEKWE KWENYE KATIBA?SWALI LA MDAU KWENYE FORUM YA KATIBA YA WATU

Historia ya Vita vya Majimaji inaonesha kuwa awali walikamatwa machifu 48 na baadaye kukamatwa wengine ambapo idadi ya machifu walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja ilifikia 66.

Mjadala kuhusu umuhimu wa elimu ya Katiba na uelewa wa sheria kwa wananchi unajumuisha masuala muhimu yanayohusu ujenzi wa demokrasia, utawala bora, na usawa katika jamii. Hapa kuna taarifa na tathmini ya kina juu ya mjadala huo: