KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (#TCD) MBIONI KUANZISHA JUKWAA LA WANAWAKE, KUTATUA CHANGAMOTO ZA SIASA NA UONGOZI.

 






KITUO cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimefanya kikao na viongozi wa Jumuiya za wanawake wa vyama wanachama wa TCD kujadili namna ya kuanzisha jukwaa la wanawake chini ya Kituo hicho.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Kituo cha Demokrasia Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Agosti 09, 2023 huku vyama; CHADEMA, CCM, CUF, ACT-WAZALENDO pamoja na NCCR - Mageuzi wakishiriki.
CHAUMMA wameshiriki kuwakilisha vyama visivyo na wabunge/madiwani.
Jukwaa hilo linaundwa ili kuwakutanisha pamoja viongozi wa Jumuiya za wanawake za vyama wanachama wa TCD kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kutatua changamoto za wanawake katika siasa na uongozi.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya utawala wa Kijerumani katika eneo la Tanganyika inahusisha kipindi cha ukoloni wa Kijerumani ambacho kilidumu kati ya mwaka 1885 na 1916

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 23 OKTOBA, 2022