MSAJILI AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA KUJADILI KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI

Mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kushoto), akisisitiza jambo mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, wakati wa kikao cha Msajili na viongozi waandamizi wa CHADEMA leo jijini Dar es Salaam. Kikao cha Msajili na CHADEMA ni juhudi za ofisi hiyo kuimarisha hali ya kisiasa hususan demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini. 

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kwanza kushoto) wakati wa kikao cha Msajili na chama cha CHADEMA chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kulia) akiteta jambo na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati), baada ya kumaliza kikao chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu John Myika. 




 

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya utawala wa Kijerumani katika eneo la Tanganyika inahusisha kipindi cha ukoloni wa Kijerumani ambacho kilidumu kati ya mwaka 1885 na 1916

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 23 OKTOBA, 2022