JE UNAJUA DELTA YA RUFIJI NDIO ENEO ZIMEZAMISHWA MELI KUBWA MBILI ZA KIVITA ZA UJERMANI?
Delta ya Rufiji. Picha kupitia panoramio.com © Bernd Zehring (https://ssl.panoramio.com/photo/802524 ) Kwa nini walikuwa wamekuja huku na walikuwa karibu kufanya nini? Washambulizi wa Biashara Baada ya kuanza Vita vya Kwanza vya Dunia, Jeshi la Wanamaji la Kifalme la Ujerumani lilikuwa na manuari nne zilizowekwa katika sehemu mbali mbali za ulimwengu. Meli hizi za kivita zilikuwa tishio kubwa kwa Uingereza kufanya biashara na zilivuruga njia zote za bishara na usafirishaji lilikuwa jambo ambalo Admiralty, Winston Churchill, kwa wazi alitaka kuliepuka. Wanamaji wa SMS Karlsruhe na SMS Dresden walikuwa nje ya pwani ya mashariki ya Mexico; katika Pasifiki kulikuwa na kikosi chenye nguvu cha wanamaji, ambacho kilijumuisha SMS maarufu Emden, ambayo ilianza safari ya ajabu na kusababisha hofu kubwa kwa meli katika Bahari ya Hindi. Wakati huo huo, pwani ya Afrika Mashariki kulikuwa na hii SMS Konigsberg. SMS Konigsberg jijini Dar es Salaam. mchoro ...