UKIUKWAJI WA HAKI NA DHURUMA NI ZAO LA SHERIA NA KANUNUNI ZA KIKOLONI NA ZINADUMU HADI LEO, TUANZE KUJIMBUSHA TUKIANZIA PWANI YA TANGANYIKA NA VITA VYA ABUSHIRI NA BWANA HERI MWAKA 1898 HUKO TANGA

 

Viongozi wake waliojulikana zaidi ni Abushiri ibn Salim al-Harthi kutoka Pangani na Bwana Heri wa Saadani.

Tukio la tarehe 15 Desemba 1889, Abushiri bin Salim, kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni Mjerumani akinyongwa hadharani na Mjerumani huko Pangani Mkoani Tanga.

Sheria ya kikoloni -Mtu alinyongwa hadharani kujaza hofu jamii, na makaburi ya viongozi hayakujulikana kuzima historia.
Vita ya Abushiri ilikuwa jaribio la wenyeji wa pwani ya Tanganyika kuzuia utawala wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki mwaka 1888/1889 lililokandamizwa na jeshi la Wajerumani. Wajerumani waliita “Uasi wa Waarabu”.
Pwani za Tanganyika na Kenya pamoja na visiwa kama Unguja au Mafia vilikuwa chini ya Omani tangu mwaka 1698 wakati Waomani waliwafukuza Wareno kutoka Mombasa.
Mnamo 1840 Sultani Said bin Sultan alihamisha mji mkuu wa utawala wake kutoka Maskat kuja Zanzibar mjini. Alidai pia ubwana juu ya miji yote ya Waswahili ilikuwepo kwenye pwani. Hali halisi miji ya Waswahili ilijitegemea kwa kiasi kikubwa vilevile makabila ya pwani na kanda la bara lililopo karibu na pwani. Lakini kwa jumla wote walikubali aina ya utawala wa juujuu wa sultani.
Katika miji muhimu Sultani aliweka maliwali au kumkubali mkubwa wa mji kuwa liwali wake. Liwali alikuwa na wajibu wa kukusanya ushuru kwa ajili ya sultani na hii ilikuwa muhimu hasa kwa mabandari ambako watumwa na pembe za ndovu walifanyiwa biashara.
 

 

 Kufika kwa Wajerumani:

Mnamo 1884 Mjerumani Karl Peters alifika Zanzibar akiwa mwakilishi wa Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani akaendelea kuvuka bahari na kufanya mikataba ya ulinzi na machifu kadhaa wa Tanganyika. Hakujaribu kufanya mikataba katika eneo la pwani lenyewe ilhali alijua ilikuwa eneo la Kizanzibari. Hata hivyo sultani alipinga mikataba akidai ya kwamba machifu hao waliwahi kukubali ukuu wake, kwa hiyo Peters alikuwa alivunja eneo la Kizanzibari.
Lakini serikali ya Ujerumani, iliyowahi kupinga mipango ya Peters, hatimaye ilikubali na kutoa waraka wa ulinzi kwa ajili ya maeneo ya mikataba ya Peters. Serikali ya Sultani ilipokataa kukubali madai yale ililazimishwa kuvumilia kwa kufika kwa manowari wa Kijerumani mbele ya mji wa Zanzibar.
Lakini madai ya Wajerumani juu ya sehemu za bara zilikuwa bure kama pwani yote ilikuwa chini ya Sultani na bidhaa zote zilifika au kutoka katika maeneo haya zilipaswa kupitia mabandari ya sultani na kupigwa ushuru hapo.


 
 
 
 
 
 
 

Comments

Popular posts from this blog