BARAZA LA MAWAZIRI LA SERIKALI YA MADARAKA YA TANGANYIKA MARA BAADA YA BARAZA HILO KUAPISHWA JIJINI DAR ES SALAAM SEPTEMBA 3, 1960.
Kutoka kushoto kwenda Kulia:
Mstari wa Mbele Waliokaa: Chifu Abdullah Said Fundikira, Waziri wa Ardhi na Upimmaji, M J Davies, Waziri wa Habari, Julius K Nyerere, Waziri Kiongozi, Sir Richard Turnbull, Gavana wa Tanganyika, J S R Cole, Mwanashria Mkuu, Sir Ernest Vasey, Waziri wa Fedha, Derek N M Bryceson, Waziri wa Afya na Kazi.
Oscar Salathiel Kambona, Waziri wa Elimu, Paul Bomani, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Ushirika, George Kahama, Waziri wa Mambo ya Ndani, Amir Habib Jamal, Waziri wa Mawasiliano, Nsilo Swai, Waziri wa Viwanda na Biashara, na Rashidi Mfaume Kawawa, Waziri wa Nyumba na Serikali za Mitaa. Kawawa na Kambona ndio waliopewa jukumu la Utekelezaji wa 'Afrikanaizesheni' mara baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Nyerere.
Comments
Post a Comment