RIPOTI YA KIKOSI KAZI KUHUSU URATIBU MAONI YA WADAU WA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA, MAPENDEKEZO 18 YA RIPOTI NA PROF. RWEKAZA MUKANDALA
1. Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote, yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi.
2. Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia baraza la vyama vya siasa linaloundwa na vyama vyenyewe mamkala ya kushughulikia swala la uvunjifu wa maadili ya vyama vya siasa kupitia kamati yake ya maadili, msajili wa vyama vya siasa aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa.
3.	Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote vyenye usajili kamili.
4.	Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu ili kuongeza uwajibikaji wa tume.
5.   Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenyekiti) jaji mkuu wa Zanzibar (M/mwenyekiti), kamishna wa serkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Tanzania bara, mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma ya Zbar, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na wajumbe 2 watakaoteuliwa na jaji mkuu wa JMT baada ya kupendekezwa na chama cha wanasheria Tanganyika na chama cha wanasheria Zbar. Pia, angalau wajumbe wawili wa uteuzi wawe wanawake, sifa za kuwa mwenyekiti, makamu au mjumbe ziainishwe, nafasi za ujumbe zitangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi
6.	Matokeo ya Rais yahojiwe kwenye Mahakama ya juu 
7.	Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, maadili, weledi, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao. Wasimamizi watakaokiuka taratibu wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
 
 
 
Comments
Post a Comment