SABABU 40 ZILIZODHIHIRISHA MAPUNGUFU KATIKA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA 2015 ZIMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU 2 (KIMCHAKATO NA KIMAUDHUI). A. MATATIZO YA KIMCHAKATO





Kupuuzwa kwa maoni ya wananchi kama yalivyoainishwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba.  Rasimu hii ya Pili iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilizunguka nchi nzima ikikusanya maoni ya wananchi lakini  maoni hayo yamepuuzwa.


Muundo wa Bunge Maalum (Kifungu cha 22 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba).  Bunge hili lilijaa wanasiasa kwani lilikuwa lina wabunge wote wawakilishi wote, hivyo kufanya idadi ya wanasiasa kuwa robotatu ya Bugne lote.  Hata wajumbe 201 nao ndani yake kulikuwa na wanasiasa 40 wawakilishi wa vyama.  Vilevile kulikuwa na wawakilishi wa AZAKI ambao pia ni makada wakongwe wa vyama vya siasa.  Suala hili lilipelekea majadiliano kufuata mlengow a kisiasa.


  Bunge la Katiba lilikosa uhalali wa kisheria na kisiasa pale lilipoendelea na majadiliano ili hali baadhi ya wajumbe walikuwa wametoka nje ya ukumbi.  Ingepaswa maridhiano yafanyike ndipo Bunge hilo liendelee.


 Upigaji wa kura; kuweka kwa makusudi kura za wazi na siri ili kuwabana wanachama ambao watakwenda kinyume na maslahi ya vyama husika.


   Kuweka kanuni ya kuruhusu upigaji kura kwa watu walioko hospital India, Hijja na kwingineko ili mradi akidi itimie.


Kutokutimia kwa Akidi za kamati mbalimbali walipokuwa wanajadili Rasimu ya Katiba.  Akidi ilikuwa haitimii kwa kuwa wabunge wengi wa Zanzibar walikuwa wametoka na UKAWA.


 Kura za maruhani; kulikuwa na kura za watu wasiokuwepo Bungeni na waliofariki.  Kwa mfano Mbunge marehemu Shida Salum wa kundi la 201 alihesabiwa kuwa amepiga kura.  Vilevile Mbunge wa Zanzibar ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi alihesabika kuwa amepiga kura ili hali hakuwepo Bungeni.


  Baadhi ya Wabunge wa Bara kuonekana wamepiga kura Zanzibar kinyume chake.  Kwa mfano Zakhia Meghji alionekana amepiga kura ya Zanzibar.



 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge maalum kubadilishwa kila kukicha ili kukidhi mahitaji ya kisiasa katika kupitisha Katiba inayopendekezwa.  Kwa mfano mwezi Desemba, 2013 Sheria ilibadilishwa ili kufuta Tume ya Mabadiliko ya Katiba.




  Kufutwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kulipelekea wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoelewa baadhi ya vifungu na kuvitafsiri tofauti


 Kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kutoka kwenye Kamati ya Uandishi.  Japo hakuelezea sababu zake za kujiuzulu kwa uwazi lakini maswali ya kujiuliza yanabaki.












Comments

Popular posts from this blog