Posts

Showing posts from February, 2023

ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT) (UMOJA KWA MABADILIKO NA UWAZI) NI CHAMA CHA KISIASA NCHINI TANZANIA.

Image
Alliance for Change and Transparency (ACT)  ( Umoja kwa Mabadiliko na Uwazi ) ni  chama cha kisiasa  nchini  Tanzania .  Kimepata  usajili  wake kamili mnamo  Mei   2014  Chama kilianzishwa mwaka wa 2014.   Kimenuia kurudisha sera za Ujamaa. Mbunge wa zamani wa upinzani Zitto Kabwe amejiunga na chama hicho mnamo Machi 2015 kufuatia kufukuzwa kwake katika chama cha Chadema. Mwaka 2015 chama kilipanga kuchukua angalau  majimbo  10 na kukusanya  asilimia  15 ya jumla ya  kura  zitakazopigwa katika  uchaguzi mkuu .

Watanzania kwa umoja wetu bila kujali itikadi za vyama, dini, ukabili au vyeo tukiungana tunaweza kusababisha mabadiliko chanya na kwa haraka kwa Taifa letu. Tusikilizane, Tulindane, Tuinuane.

Image
 

"TAIFA LA WOTE, MASLAHI YA WOTE”

Image
#brandpromiseAct2023

Historia ya Vita vya Majimaji inaonesha kuwa awali walikamatwa machifu 48 na baadaye kukamatwa wengine ambapo idadi ya machifu walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja ilifikia 66.

Image
Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ni eneo ambalo limehifadhiwa vizuri na serikali ili kuwawezesha watu kujifunza kumbukumbu nyingi ambazo ni kivutio adimu cha utalii wa kishujaa na kiutamaduni.  Watu  kutoka mkoa wa Ruvuma na  nje ya nchi wanatembelea eneo hili maarufu katika historia ya Tanzania hasa katika harakati ambazo zilifanywa na babu zetu kupambana na wakoloni ili kujitawala wenyewe bila kunyonywa. Mkurugenzi wa  makumbusho ya  Taifa ya Majimaji mhifadhi Kiongozi Balthazar Nyamusya anasema  eneo hilo la makumbusho lina historia tatu ambazo ni historia ya vita vya majimaji,historia ya ujio wa wangoni kutoka Afrika ya Kusini na  historia ya uhuru wa Tanganyika.  Anaitaja historia ya vita vya majimaji ililenga kumkomboa mtanzania kutoka mikononi mwa wakoloni Wajerumani na kwamba sio sahihi kuwa vita hiyo ilikuwa na uwezo wa kugeuza risasi kuwa maji bali ililenga kuwapa nguvu wapiganaji kujitolea hata ikibidi kupot...

ISEMAVYO SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA,2017

Image
 Chimbuko la sheria hii lilitokana na uhitaji mkubwa wa kuwa na sheria nchini itakayoongoza kisheria namna ya utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wahitaji ili waweze kufikia haki. Sheria hii ilitungwa na bunge mnamo tarehe 31 Januari, 2017, ikapitishwa rasmi na kusainiwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 21 Februari, 2017. Ilitanganzwa kwenye gazeti serikali namba 9 la 2017 na kuanza kutumika rasmi tarehe 1 Julai, 2017 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 20 la mwaka 2017. Pia sheria hii imetungwa kukidhi matakwa ya mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo nchi yetu imesaini na kuridhia kuhusu haki za binadamu ikiwemo haki ya kupata msaada wa kisheria. “Mtu anayesaidiwa” maana yake ni mtu anayepatiwa msaada wa kisheria chini ya sheria hii. “Mtu asiye na uwezo” Maana yake mtu asiye na uwezo wa kumudu gharama za wakili wa kujitegemea ikiwa ni pamoja na makundi mengine ya watu kama itakavyohitajika kwa maslahi ya utoaji haki. “Ushauri wa ...

FAHAMU HISTORIA YA MJI WA SONGEA ULIONZISHWA MWAKA 1897

Image
Muonekano wa mji wa Songea mwaka 1897  Mashujaa 67 wa vita ya Majimaji ambao walinyongwa na wajerumani mwaka 1906 kisha kuzikwa ndani ya makumbuisho ya Taifa ya Majimaji ambako kuna makaburi mawili,kaburi kubwa ni la mashujaa 66 ambao wamezikwa pamoja na kaburi moja ni la Jemedari wa wangoni Nduna Songea Mbano  Jemedari wa Kabila la wangoni Nduna Songea  Mbano ambaye jina lake limepewa mji wa Songea,picha hiyo alipigwa na wajerumani mwaka 1906 muda mfupi kabla ya kunyongwa na wajerumani Mnara ambao umejengwa katika eneo la Songea Club mahali ambapo walinyongwa kikatili na wajerumani mashujaa 67 mwaka 1906 kisha kwentda kuzikwa ndani ya makumbusho ya Majimaji Mahenge Songea Katikati ni  Chifu wa Tano wa Kabila la wangoni Nduna Imanuel Zulu Mbano akiwa ndani ya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea MJI wa Songea uliopo katika Mkoa wa Ruvuma  ni miongoni mwa maeneo machache hapa nchini ambayo yana hazina kubwa ya utajiri  wa kihistoria ...

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) LAKEREKA SHERIA KUTOREKEBISHWA, LAMWOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI

HISTORIA YA KATIBA YETU

Image
Kwa mujibu wa wataalamu wa sheria kutoka chuo cha sheria cha Tanganyika(Law School of Tanganyika) Tanzania, katiba inahitaji kupitiwa mara kwa mara kuhakikisha kua inaakisi era za kidiplomasia pamoja na kwenda na wakati. Katiba ikigundulika(kwa minajili ya mapekuzi na machunguzo yakinifu) kuwa haikidhi mahitaji hayo au ikibainika kuwa ina mapungufu tume maalumu ya wataalamu wa sheria(law scholars) huundwa ili kupitia na kuirejeza kwenye ukisasa(relevance restoration).  KATIBA YA UHURU Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1961 ilitokana na azimio la sheria ya uhuru (Order in Council) lililopitishwa katika Bunge la Uingereza na kuletwa Tanganyika kama Katiba ya awali. Katiba hii ilitengenezwa na waingereza nchini Uingereza na kuletwa kwetu. Hata hivyo Katiba hii ilikuwa na mapungufu kadhaa kubwa ikiwa mambo mengi ya kutegemea kufanyiwa maamuzi toka Uingereza chini ya Malkia ambaye ndiye alikuwa mkuu wa nchi yetu. KATIBA YA JAMHURI Utengenezaji wa katiba hii haukuhusisha wananchi wa ka...