Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Alhamisi mjini Dar es Salaam alimtaja Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kama 'bingwa' wa demokrasia


Machi 2021 alikua mwanamke wa kwanza kuiongoza Tanzania. Dr.Samia Suluhu Hassan amemrithi  rais John Pombe Magufuli aliyefariki dunia ghafla.

Katika ziara yake Makamu wa rais wa Marekani wakati wa mazungumzo na Rais. Samia Suluhu Hassan, amemwita "bingwa", kuhusu demokrasia, utawala bora, ukuaji wa uchumi wa muda mrefu na mgogoro wa Tabia nchi. "Katika suala la ukuaji wa uchumi, utawala bora unatoa utabiri, utulivu na sheria ambazo biashara zinahitaji kuwekeza," Kamala Harris amesema.

"Kuna uwezekano wa kukua hapa," ameongeza. Akiweka shada la maua katika kumbukumbu ya shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, ulioshambuliwa mwaka 1998 kwa wakati mmoja na ubalozi wa Marekani nchini Kenya, jijini Nairobi.

Ziara ya Kamala Harris ni sehemu ya juhudi za Washington kuimarisha uhusiano wake na Nchi za Afrika ikitajwa kama makabiliano na ushawishi wa China na Urusi kwa Nchi za Afrika.

Machi 19, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza miaka miwili mamlakani  Mwezi Januari, alitangaza kufuta zuio la mikutano ya kisiasa na kufungua njia ya kurejea nchini kwa viongozi wa upinzani kama vile Tundu Lissu na Godbless Lema, Mwanzoni mwa mwezi Machi, alikuwa ameahidi kuzindua upya mchakato wa marekebisho ya katiba, madai ya zamani ya upinzani.


 

Comments

Popular posts from this blog