Mnara wa ukumbusho wa kuvutia zaidi kwa wahasiriwa wa Kiafrika wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu (1914-1918) haupatikani barani Afrika bali uko Ufaransa.
Katika vita vya Delville, moja ya mapigano makali katika eneo la Somme mwaka wa 1916, Brigade ya 1 ya Infantry ya Afrika Kusini ilipata hasara kubwa na waafrika wengi waliuwawa.
Jeshi la Afrika Kusini ni mojawapo ya mashirika machache barani Afrika ambayo yanaheshimu na kuthamini mchango wa Askari Hawa waafrika.
KUNA ufahamu mdogo kuhusu vita ya kwanza ya Dunia miongoni mwa watu weusi wa Afrika, hili limefanywa kusudi na wakoloni wa Afrika ili Historia hii isisimuliwe kabisa kwa uzao wa baadae wa Kizazi cha Afrika
WAKATI wa mzozo huo, takriban watu milioni 2 kutoka kote barani Afrika walihusika kikamilifu katika makabiliano ya kijeshi, kama wanajeshi au wabebaji mizigo, huko Ulaya na Afrika. Mwanzoni mwa vita, baadhi ya Waafrika walijitolea kushiriki, wakitiwa moyo na kudanganywa juu ya matarajio ya mapato ya kawaida.
Kuanzia 1915, Wazungu walianza kuandikisha maelfu ya wanaume Waafrika. Wafaransa pekee walitumia wanajeshi wa Kiafrika 450,000 kutoka makoloni yao Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kupigana dhidi ya Ujerumani kwenye mstari wa mbele huko Ulaya.
Waafrika Milioni moja waliuawa Afrika Mashariki pekee
Vita vilipozuka Ulaya mwaka wa 1914, askari wa Kiingereza na Ufaransa walijitayarisha kuteka makoloni manne ya Wajerumani katika Afrika (Afrika Mashariki ya Kijerumani, Afrika Kusini-Magharibi ya Kijerumani, Togoland na Kamerun).
Mapigano yalikuwa ya kikatili mno,haswa katika Afrika Mashariki ya Ujerumani ambapo Jenerali mkatili wa Ujerumani Lettow-Vorbeck alipitisha mkakati wa kuasi , kuteka na kuuwa katika maeneo mengi zaidi katika vita. Zaidi ya wabebaji 200,000 walisafirisha silaha, risasi na chakula kwa wanajeshi. Wakijulikana kwa jina "Askari mwaminifu" (neno la Kiswahili la 'askari') bado limebaki katika vitabu vya historia ya Ujerumani.
Kwa kweli kulikuwa na Uonezi wa ajabu
watu wengi walidakwa kutoka katika himaya zao na walidharauliwa na wakazi wa wenzao baada ya Kurudi nyumbani kutoka katika vita, walikosa mashamba. Mavuno yaliporwa na kuharibiwa na wanajeshi waliokuwa wakipita ili kuhakikisha kwamba hakungekuwa na chakula chochote kwa ajili ya wanaowafuatia.
Hakuna takwimu sahihi zinazosema ni watu wangapi walikufa kwa njaa. Ukweli kwamba eneo la utawala wa kikoloni la Dodoma katika eneo ambalo sasa ni Tanzania lilipoteza asilimia 20 ya wakazi wake mwaka 1917/18 ni jambo hadi leo limeacha dalili fulani ya unyonge na sononeko kwa jamii ya kitanzania.
Wanahistoria wanakadiria kuwa watu milioni moja walikufa Afrika Mashariki kutokana na vita hivyo. Mlipuko wa homa ya Kihispania, ambayo ilienea haraka, watu waliodhoofika muda mfupi baada ya vita kumalizika, ilisababisha vifo zaidi ya 50,000 hadi 80,000.
"Vita vilibadilisha baadhi ya maeneo kwa kiasi kwamba yalihitaji miongo kadhaa kupona, hadi sasa athali zipo,” alipata kusema Jürgen Zimmerer, profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha Hamburg.
Tanzania ya leo, iliyounda sehemu kubwa ya koloni la zamani la Afrika Mashariki ya Kijerumani, vita vya 1914-1918 kwa kiasi kikubwa havipo kwenye fahamu za Watanzania.Kizazi cha sasa kimesukumwa mbali na history hii"Ni kumbukumbu ambayo inazidi kutoweka, Wahusika wakuu wamekufa kwa muda mrefu. Walikuwa babu na bibi zetu!”
kuanguka kwa himaya za kikoloni kunahusishwa na mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia." Ilikuwa ni kuenea kwa vuguvugu la uhuru wa mataifa ya Afrika kulikoanza mwanzoni mwa miaka ya 1950 ambako kuliwakilisha mabadiliko ya kweli na ambayo sasa yanaadhimishwa na sherehe za ukumbusho na sikukuu za kitaifa kukiwa bado na kovu baya lililojificha na Siasa,sheria na mitazamo ya Kikoloni.
Vita Kuu ya Pili ya Dunia haiitaji sana Afrika kwa sababu historia kubwa lilikuwa ushindi kwa ujumla wa wakoloni huko ulaya ikiacha sehemu moja tu ya historia ndefu ya ushindi wa kikoloni na vitendo vya kikatili vilivyofanywa kwa watu wa Afrika wakati wa ukoloni.
Katika muda wa miaka 75 ambayo Ubelgiji pekee ilitawala Kongo, watu milioni kumi walikufa. cha ajabu ni vita moja tu kati ya nyingi ndio zinatajwa sana," Zimmerer anasema. "Ukoloni ulikuwa wa kikatili kiasi kwamba idadi kubwa ya watu milioni moja haivutii hisia ambayo inapaswa - au ingetokea katika mazingira ya Ulaya.”
Ulaya pia inachukulia mtazamo huu na kwa ujumla inapuuza mateso ya mamilioni ya Waafrika katika Vita vya Kwanza vya Dunia. Kwa maneno ya Zimmerer, vita barani Afrika "kwa ujumla huchukuliwa kama mzozo mdogo ambao hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa ama kuteseka.”
Nijambo linalosikitisha sana.
Comments
Post a Comment