TAWI LA TANU MTAA WA JARIBU MAGOMENI MAPIPA MWAKA 1954 CHIMBUKO LA VUGUVUGU YA KUDAI UHURU
Tawi hili la TANU Magomeni Mapipa lilikuwa na nguvu na viongozi mashuhuri wa TANU walifika mara nyingi kuzungumza na wanachama na viongozi wao. |
Ali Msham aliyekaa kati shati jeusi na wanachama wa tawi la TANU Magomeni, ni siku wanachama wa TANU walipokusanyika kwenye tawi kufanya dua kwa ajili ya safari ya Mwalimu Nyerere Kwenda UNO 1955. |
Ofisi ya #TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa kama ilivyokuwa ikionekana katika miaka ya 1950 ikiwa imezungikwa na wanachama wake. |
Kushoto: John Rupia, Julius Nyerere, Zuberi Mtemvu Waliosimama nyuma yao ni BANTU Group Vijana Walinzi wa Viongozi wa TANU |
Ulikuwa mwanzo wa safari za Mwl Nyerere kwenda majimboni na katika Kitabu cha
Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," ameeleza juu ya mkakati wa kisiasa,kikabila na kidini ulivyoratibiwa na Wazee hawa
Mkakati wa viongozi wa TAA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilikuwa TANU
iongozwe na Mkristo ili kuzimua Uislam uliogubika harakati za kupambana na
ukoloni.
Hofu ilikuwa kuzuia TANU kuonekana chama cha Waislam na harakati za kudai uhuru
ni harakati za Waislam.Hii ingesababisha kukosekana kwa umoja wa wananchi wote dhidi ya ukoloni,kubwa ilikuwa kuzuia kuundwa chama ambacho Wakristo watajitambulisha
kuwa ndiyo chama chao.
Kisha Mwalimu akaenda majimboni.
Safari yake ya kwanza alikwenda Morogoro akiongozana na Zuberi Mtemvu.
Baada ya hapo Lindi akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe na alifatwa hapa Dar es
Salaam na Ali Mnjawale na SAlum Mpunga.
Lindi akapokelewa na wana mji akina Suleiman Masudi Mnonji, Yusuf Chembera,
Mussa Lukundu, Salum Mpungana na Ali Mnjawale.
Tanga akapokewa na akina Hamisi Kheri, Mohamed Kajembe.
kumbukumbu pia zinapatikana katyika kitabu cha Abdul Sykes.
Comments
Post a Comment