Skip to main content

UN YASISITIZA UHURU WA HABARI DUNIANI


"Uhuru wowote ule unategemea uhuru wa Habari." Hii ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
 






 "pamoja na umuhimu wa Habari, lakini katika kila kona ya dunia uhuru wa Habari unashambuliwa.

Katika kuhakikisha dunia inakuwa salama Guterres ameutaka ulimwengu kusimama na  wanahabari wanaosimamia ukweli.

Aidha amezihimiza serikali kufanya  kila lililo ndani ya uwezo wao kusaidia uhuru wa vyombo vya habari, ambao kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaja kama ni msingi wa jamii za kidemokrasia. 

Ikumbukwe kuwa kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya Uhuru wa Habari duniani ni leo na kwa Tanzania, maadhimisho ya siku hiyo yanafanyika Zanzibar, ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi yakiwa na kauli mbiu ya Kuunda mustakabali wa uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha Hali za binadamu.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya utawala wa Kijerumani katika eneo la Tanganyika inahusisha kipindi cha ukoloni wa Kijerumani ambacho kilidumu kati ya mwaka 1885 na 1916