MKUTANO WA KAMATI YA UONGOZI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA JULAI 31, 2023,
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa mara baada ya kumaliza kikao cha kamati hiyo jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Annamringi Macha, Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Juma Khatib na kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mzee John Momose Cheyo. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. (Picha na ORPP) Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vya Siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Momose Cheyo akichangia mada wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika tarehe 01 Agosti 2023 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. Wajumbe w...