|
Baadhi ya wataalam kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha ACT – Wazalendo Zanzibar mara baada ya kumaliza zoezi la uhakiki wa chama hicho katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu zilizopo Vuga Mjini Magharibi. |
|
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo Kazi (wapili kushoto) akisoma moja ya nyaraka za chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembelea katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Zanzibar zilizopo Vuga mkoa wa Mjii Magharibi Zanzibar tarehe 09 Agosti, 2023. Wengine ni viongozi wa chama hicho Zanzibar na kushoto kwake ni Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bibi. Grace Mushi. |
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo akionyesha Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Alliance for Change and transparency (ACT – Wazalendo) mahususi kwa ajili ya upande wa SMZ wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama walipotembelea katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Zanzibar zilizopo Vuga mkoa wa Mjii Magharibi Zanzibar tarehe 09 Agosti, 2023. Kushoto ni Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bibi. Grace Mushi.
|
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo pamoja na Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bibi. Grace Mushi wakikagua taarifa za fedha za ACT – Wazalendo ikiwa ni sehemu ya zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa lililoanza terehe 09 Agosti, 2023 visiwani Zanzibar. Zoezi la uhakiki linafanyika visiwani humo baada ya kuhitimishwa katika Ofisi za vyama hivyo zilizoko upande wa Tanzania Bara kwa lengo la kutathmini hali ya utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria ya gharama za uchaguzi.
|
Comments
Post a Comment