|
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Ahmed Ally Akiteta j Mrajisi wa Asasi za Kirai Zanzibar, Mohamed Abdallah pamoja na mjumbe mwalikwa kutoka asasi ya kiraia YPC, Martine Mang’ong’o mara baada ya kumaliza Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 2023. (Picha na: ORPP) |
Msajili wa Vyama vya Saisa, Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe mara baada ya kumaliza Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 2023. |
|
Mwakilishi wa Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini akichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 2023. |
|
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe akichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 2023. Mkutano huo maalumu umewashirikisha baadhi ya viongozi wa dini na wawakirishi kutoka katika Taasisi za kirai kwa lengo la kujadili namna bora ya utengamano baina ya siasa na dini nchini. |
|
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi - CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba akichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 2023. |
|
Msajili wa Vyama vya Saisa, Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Prof. Alexander Makulilo ambaye alikuwa mtoa mada kuhusu matumizi ya viongozi wa dini katika siasa, mavazi na vitendo vya walinzi wa vyama pamoja na matumizi ya lugha katika mikutano wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya washiriki wa mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini wakifuatilia mada kuhusu matumizi ya viongozi wa dini katika siasa, mavazi na vitendo vya walinzi wa vyama pamoja na matumiz ya lugha katika mikutano wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. |
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Prof. Alexander Makulilo akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya viongozi wa dini katika siasa, mavazi na vitendo vya walinzi wa vyama pamoja na matumiz ya lugha katika mikutano wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
|
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ndg. Juma Khatib akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa ulifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Mkutano huo maalumu umewashirikisha baadhi ya viongozi wa dini na wawakirishi kutoka katika Taasisi za kirai kwa lengo la kujadili namna bora ya utengamano baina ya siasa na dini nchini. |
|
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akizungumza wakati ufunguzi wa Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa ulifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo maalumu umewashirikisha baadhi ya viongozi wa dini na wawakirishi kutoka katika Taasisi za kirai kwa lengo la kujadili namna bora ya utengamano baina ya siasa na dini nchini. |
Na Mwandishi wetu
Jijini Dar es Salaam, Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania liliitisha mkutano wa dharura kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa nchini. Mkutano huo ulifanyika na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, na wadau wengine.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha ADA-TADEA, alieleza kuwa mkutano huo ulikuwa muhimu kutokana na hali ya siasa ilivyokuwa nchini. Aliongeza kuwa walitaka kujadili mambo muhimu ya kitaifa na kutafuta njia nzuri ya kuunganisha nguvu na kusonga mbele kama taifa.
Katika mkutano huo, mada kadhaa zilijadiliwa, zikiwemo masuala yanayohusiana na vyama vya siasa kutumia viongozi wa dini katika shughuli za kisiasa, mavazi yanayovaliwa na vitendo vya walinzi wa viongozi wa vyama, na namna ya kusimamia mali za vyama hivyo. Mada nyingine zilikuwa ni kuhusu lugha inayotumiwa katika mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na shughuli nyingine za kisiasa.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alihimiza washiriki wa mkutano huo kutofautisha kati ya kuhoji na kutoa tuhuma. Aliwataka kujadili kwa uwazi na kistaarabu ili kuleta ushindani mzuri katika siasa na kuhakikisha amani inadumishwa nchini. Alibainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maendeleo nchini.
Hali ya kisiasa nchini Tanzania imekuwa tete kutokana na mjadala wa uwekezaji katika sekta ya bandari ya nchini. Uwekezaji huo unatazamiwa kufanywa na kampuni ya DPW inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Wapinzani wa uwekezaji huo, hususan viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekuwa wakitoa kauli za ukosoaji, hata kufikia kutoa matusi kwa viongozi wa serikali, ikiwemo Rais Samia.
Mkutano huu ulinuia kutafuta njia za kuleta umoja na kuhimiza mazungumzo ya kistaarabu ili kupunguza mvutano wa kisiasa na migogoro. Lengo lilikuwa ni kuhakikisha amani na maendeleo yanaimarika nchini kwa kuheshimu tofauti za kisiasa na kuendeleza demokrasia ya vyama vingi.
Comments
Post a Comment