MKUTANO HUU UMEKUWA WENYE TIJA KWANI MMETOA MAONI KWA KUZINGATIA MASLAHI MAKUBWA YA NCHI YETU - MHE. DOTO BITEKO
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaungana na watu wengine waliosema hapa nami nitoe shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa Juhudi zake ameweza kuimarisha ustawi wa Demokrasia hapa nchini sambamba na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuwaletea maendeleo Watanzania"
"Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amekuwa mfano wa kuigwa kitaifa na kimataifa kuhakikisha Demokrasia yetu inazidi kustawi na kuifanya Demokrasia yetu kuendeshwa kwa misingi ya haki, utawala bora na kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea na bila kusahau mazingira ya watu ambao bila wao Serikali haipati uhalali"
"Mkutano huu si mali ya Serikali kwasababu katika yaliyojadiliwa haswa kwenye hii miswaada mitatu kwa taratibu zetu za utawala bora baada ya mswaada kusomwa bungeni basi mswaada ule ni mali ya bunge na si serikali tunabaki kama wadau wengine"
"Baada ya haya yote mliojadiliana, mchukue nafasi kuitikia wito wa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye amealika wadau mbalimbali kwenda Bungeni kutoa maoni yao kuanzia tarehe 6 - 10 Jijini Dodoma, msiache kwenda na haya mliyozungumza naamini mmejifua vizuri, mmepata focus kama vyama vya siasa, naoni yenu yanazingatiwa na Serikali kwa umuhimu wa kuzingatia utawala bora unaozingatia mihimili yetu ya dola"
Mhe. Doto Biteko
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Nchini.
Comments
Post a Comment