NINI NAFASI YA SERIKALI, ASASI ZA KIRAI,
VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HIZI R4 NA NINI
KIFANYIKE
Bw. Salim.
Niliposema 'reform’ sikuwa na maana tuanze na reform. Hivyo ni lazima tuanze na maridhiano na kuvumiliana. Nakubaliana na wote wanaosema kuwa R4 ni falsafa sahihi sana. Hii mimi ninaamini kuwa hii itakuwa ni ‘legacy’ kwa mama Samia. Nini kifanyike, tuione Serikali ikifanya kwa vitendo, hili sio suala la kisiasa. Tunaona mabadiliko kwenye mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali. Ingawa kwenye siasa kuna mkwamo kwenye Sheria za Uchaguzi na Katiba mpya. Asasi za kiraia ziwaeleze wananchi na kuwafundisha.
Bw. S.Wasira.
Vyombo vya Habari vifanye kazi yake ya kuelimisha umma kwakuwa vinasilikizwa na Wananchi. Nafasi ya Serikali ni haya yanayoendelea, Serikali iko kwenye usahihi. Tutazame ‘reforms’ kwenye maeneo yote kwa mfano elimu, vyama vya siasa vina nafasi ipi.
Bw. Ado - ACT WAZALENDO.
Mchakato wa Katiba nchi siyo jambo la kusubiri, mchakato wa Katiba mpya na ukamilike mapema baada ya uchaguzi mkuu. Mhe. Rais hakuwa na shinikizo lolote baada ya kichapo cha mwaka 2020, kwa hiari yake akaamua kufanya mabadiliko. R4 itapimwa kwa vitendo, kila mmoja wetu ana wajibu. Ingawa yako mambo ambayo yameshajenga mambo ya kitaifa. Sisi kama ICT Wazalendo tumechambua mambo ambayo yameshatekelezwa. Mengi yapo kwenye ripoti ya kikosi kazi, hivyo yaendelea kutekelezwa.
Bi. Mongela.
S5 za Japani zimewezesha maendeleo ya Japani. Hivyo na hili la R4 tunapaswa kufanyia mkamkati, tunapaswa kuitengenezea dira ili iwe ya Taifa. Tumuombe Mhe. Rais tulitoe mkononi mwa Mhe. Rais kisha tukimbiee nalo. Mimi natoa mapendekezo hizi R4 ziwe za umma na ziweze kwenda hata kwenya familia. Naomba kuwe na muendelezo ya kufikisha kwa kila mtu yaani Methodolojia, tukumbatie vile ambavyo tumeshavifanyia kazi.
Bw. Doyo.
Naomba kuungana na Mhe. Lipumba, ni vema wenzetu wa Serikali wakalichukua hili. Kuhusu ajenda 2063, Mhe. Rais ameruhusu mwanamke aongoze mwanamke mmojammoja kwenye baraza ili washiriki kisheria. Nawaomba tutumie R4 kwenye mjadala huu.
Comments
Post a Comment