UFAFANUZI WA 4R KAMA ULIVYOONGOZWA NA BW. ABBAKARI MACHUMUMWONGOZA MADA(SIKUYA 01)
"Misingi ya R4 yameendelea kubadilika sura kutokana na nyakati. Tatizo kubwa nikuelewa mahusiano yetu sisi kama Watanzania. Mhe. Rais sasa anataka tuzungumze na turidhiane. Mhe. Rais amechukua hatua stahiki, hata vyombo vya habari sasa vinaendelea kufanya kazi kwa uhuru. Kwa hivi sasa uchumi wetu ni endelevu. Hapa Tanzania bado tunaishi kijamaa japo hatuwezi kuuona. Hivyo chakwanza ni maridhiano ya kimfumo na unapaswa kuwa endelevu"
Bi. Mongela
Maridhiano, hizi R4 mwisho wake tutaweza kubadili fikra zetu. Hivi sasa ukiangalia ni kama tumekuwa wanaharakati ni kama vile nchi yetu haijapata uhuru. Mabadiliko ya Tehama ni mabadiliko makubwa sana. Hivi sasa tunapaswa kujipanga kimawazo kwakuwa sasa kuna ‘artificial intelligence’. R4 zitusaidie kujenga nchi yetu.
Kuhusu Maendeleo Endelevu, msipofanya maridhiano mtakuwa hakuna muda wakutafakari, tunapaswa kwenda kweye maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mifumo yetu ya Elimu, Siasa, Utamaduni n.k inapaswa iendane na uchumu wetu.
Comments
Post a Comment