UFAFANUZI WA 4R KUTOKA KWA
WADAU MBALIMBALI
KATIKA MREJESHO WA
MKUTANO WA MSAJILI
WA VYAMA VYA SIASA
Bw. Doyo.
Naomba nianze na nia ya Mhe.Rais, nianze na Watendaji wa chini. Serikali itengeneze programu maalum yakuwafanya hawa Watumishi wa Serikali wazielewe vizuri R4. Dira ya Taifa ikieleweka tutapata Wawekezaji pia. Mhe. Rais anasisitiza kusikilizana na kutuvumilia. Hivyo kuna umuhimu watendaji wawe na uelewa.
Bw. Salim
Kwa kiwango gani R4 zinaweza kuisadia kuendana na Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda za 2063. Haya yote yanapaswa yaangaliwe na nguzo za kidunia, ili dunia itupime hivyo. Kama kuna joto kubwa la kisiasa hautaweza kufikia kwenye haya maendeleo. Reforms zinazozungumzwa hapa ni pamoja na kuvumiliana kwa hoja ilituweze kuitengeneza nchi yetu, tunapaswa kuja na reforms za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivyo tuweze kupimana kwa uvumilivu na ukweli.
Bw. Ado Said
Falsafa hii ikitekelezwa kwa ukamilifu basi tutaenda sambasamba na Ajenda ya 2063 na Maendeleo Endelevu ya 2030. Maridhiano ni sawa, ila nguzo mama ni Mabadiliko. Ni lazima sasa hii nguzo mama hii iendane na nguzo ya Katiba Mpya, Mchakato wa Katiba Mpya uanze hivi sasa na kuweka misingi madhubuti ya kisheria. Pamoja na kujadili miswada hii, lakini bado hatuna kalenda za utekelezaji wa Tume ya Haki Jinai na Kikosi Kazi, tunataka kuwa na kalenda, tunahitaji muafaka wa kitataifa. Mambo ambayo yameshapata muafaka wa kitaifa badi yatekelezwe. Kuhusu mifumo ya ruzuku bado ina shida, hivyo tufanye mabadiliko ya kimfumo. Tuwe na Kalenda ya utekelezaji.
NAFASI ZA R4 KULETA UTENDAJI MZURI WA HALI YA KISIASA
Bw. Ado
Mhe. Rais amezichukua hizi R4 kama nyenzo yake muhimu yakufanyia kazi. Maboresho ya kisiasa yaweze kukidhi haja ya Watanzania wote. Kwakiasi gani Wananchi wanaulewa kuhusu R4 za Mhe. Rais;
Sisi Wanasiasa tumeleewa vizuri sana kuhusu 4R na ndio maana tumekuwa tukishiriki kwenye meza ya mazungumzo. Hivyo hata uwepo wetu hapa unaonesha kuwa kumeelewa vizuri kuhusu hii R4. Mhe. Rais ametuonesha utashi wake na sisi tumeonesha kuwa tunamuamini. Hivyo tujenge misingi imara ya kikatiba na kisheria.
Bw. Salim.
Wananchi hawataki kuelewa kuhusu R4 ila wanataka kuona matokeo ya R4. Hivyo nguzo kuu ni Reforms, hivyo tunahitaji matokeo ya R4 na siyo mahubiri yake ya R4. Matokeo kwenye uchumi, ajira ubora wa elimu, tija ya kiuchumi, umasikini wa kipato unapungua. Tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa kisiasa, tuwe na tume huru, kujenga ,msingi wa kitaifa kuhusu kuwa na Katiba Mpya. Hivyo Watanzania tunaweza kuanza kukata tamaa. Dhamira ipo, hivyo tumsaidie mwenye dhamira ili tupate matokeo. Hivyo wananchi wataelewa baada ya kuona matokeo.
Bw. Doyo.
Kama unadai mkono na ukarudishiwa kodle basi utashukuru. Lapili, Watanzania hawa wanaelewa sana R4 za Mhe. Rais, kabla ya R4 kulikuwa na Mahabusu ambao walikuwa wanaonewa. Hivyo tuipongeze Serikali kwa kupeleka hii miswada kwa njia ya kawaida, kama ambavyo Mhe. Waziri amesema kuwa tutapokea maoni yote ya Wadau. Wote tumeona kuwa mada ni kujadili ajenda. Hivyo tunaomba tuweke maoni yetu sasa. Hata kuruani hakiundikwa kwa siku moja, tunapaswa tuige mifumo ya kiroho, haya mambo ni mchakato.
Bi. Mongela.
Naomba nitumie mfano wa kutaka mabadiliko ya katiba, aya ya 12 na 13 imesema Binadamu wote ni sawa, hivi hii katiba itaniondelea hayo. Mfano mwingine wakati ule wa Rais wa Kwaza wa Taifa hili, Rais alikuwa anazungumzia kuhusu utofauti wa kipato. Ni lazima tujue hiyo katiba itaandikwaje, mkakati wake ukoje na italiwekaje suala la usawa wa Mtanzania.
Jambo lingine ni hili la R4, juzi nimewaeleza kuwa naenda kwenye R4 watu walikuwa wananishangaa, hizi R4 ziwe za Mtanzania na zisiwe na Mama Samia. Tunapaswa tutumie Kiswahili, bado tuna kazi yakuwaelimisha Wananchi kuhusu R4.
Bw. S.Wasira.
Uelewa wa Wananchi kuhusu R4.
Nimesisitiza kuhusu Maridhiano (Recolianciation) ili turidhiane kwanza ndipo tufanye mabadiliko. Ni ngumu kuwa na ratiba yenye tarehe kwenye mambo makubwa ya nchi. Ni muhimu kuzungumza kuhusu Ustahimilivu (Resiliency), kuhusu Katiba hatuwezi kuwa na tarehe ya upatikanaji wa Katiba. Tutoe maoni yetu ilĂ ‘minimum reforms’ ifike mahali, tunapaswa kuwa na mchakato wa muda mrefu, mfupi na wa kati. ‘Reform’ haiwezi kutupatia majibu kesho.
Comments
Post a Comment