RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Balozi mstaafu Ali Siwa amekuwa katika utumishi wa umma tangu mwaka 1977 na kuweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Kati ya mwaka 2001 mpaka 2014, Balozi Mstaafu Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje, Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani. Mwaka 2014, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, alimteua Ndugu Ali Idi siwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kigali, nchini Rwanda, nafasi aliyoihudumu mpaka mwaka 2018 September 2018, aliteuliwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini NSSF, nafasi ambayo alikuwa anaitumikia mpaka mwaka 2023. .