Posts

Showing posts from January, 2024
Image
  TATHIMINI MJADALA HUU UNAHUSU MASUALA MUHIMU YA KISIASA, KISHERIA, NA KIJAMII YANAYOHUSIANA NA UWAJIBIKAJI WA SERIKALI NA VIONGOZI.   Hii ni tathmini na maoni kuhusu mambo kadhaa yaliyotolewa katika mjadala: Muundo wa Katiba na Uwajibikaji: Ni kweli kwamba katiba inaweza kuwa msingi wa kuanzisha mfumo wa uwajibikaji. Ibara inayohusu uwajibikaji inaweza kuwa na jukumu muhimu katika kuainisha madaraka na majukumu ya viongozi. Hata hivyo, kama ilivyosemwa, utekelezaji wa kifungu hicho ndio muhimu zaidi. Mapungufu ya Uwajibikaji: Kuchambua mapungufu katika uwajibikaji ni hatua muhimu. Ni vizuri kuzingatia mifumo yote inayohusika, pamoja na katiba, taasisi za serikali, mfumo wa kisheria, na utamaduni wa kijamii. Hii inaonyesha umuhimu wa kutazama jumla ya mfumo wa utawala. Uwajibikaji wa Viongozi na Wananchi: Hoja ya kudai katiba mpya ili kufanikisha uwajibikaji ina mantiki. Hata hivyo, ...
Image
MJADALA [14:55, 20/01/2024] +255 769: Tudai katiba mpya ITAKAYO wafanya watawala wa wajibike kwa wananchi MAJIBU [00:51, 21/01/2024] T: Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba mafanikio ya uwajibikaji wa serikali na viongozi yanaweza kutegemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na muundo wa katiba na utekelezaji wake. Ni kweli Katiba inaweza kuwa msingi wa kuanzisha mfumo wa uwajibikaji. Inaweza kuainisha madaraka na majukumu ya viongozi, kuhakikisha uwazi wa shughuli za serikali, na kutoa njia za kudhibiti mamlaka. Hata hivyo, hata katiba nzuri inaweza kushindwa kufikia lengo lake ikiwa hakutakuwa na utendaji mzuri wa taasisi za serikali, uwajibikaji wa kijamii, na mfumo mzuri wa kisheria. Ibara inayohusu uwajibikaji katika Katiba ya Tanzania inaweza kuwa Ibara 9. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kwamba mafanikio ya uwajibikaji hayategemei tu kwenye kifungu hicho bali pia utekelezaji wake katika mazoezi ya kila siku. Kwa kuzingatia haya, ikiwa kuna mapungufu katika uwajibikaji, ni muhimu kutathmin...
Image
TATHIMINI YA KINA JUU YA MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA, UKIFAFANUA MJADALA MZIMA JINSI WADAU WALIVYOTOA NA KUCHANGIA MAWAZO YAO JUU YA MADA ILIYOWEKWA MEZANI  (SIKU YA PILI) UFUNGUZI   Mkutano ulianza na ufunguzi uliofanywa na Mhe. Othman M. Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao kilianza na salaam za utangulizi na viongozi mbalimbali, ikijumuisha Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu.  Mada kuu ya kikao ilikuwa mswada wa sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, na matokeo ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika awali.   Maoni ya Wadau Wadau mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu mswada huo. Bw. Majaliwa Kyala aliipongeza Serikali kwa kuondoa kifungu cha mgombea binafsi na kuelezea umuhimu wa kusimamia uchaguzi wa Serikali ya Mitaa.   Bi. Nuru Kimwaga aliipongeza Serikali kwa kuwaunganisha wanasiasa na kutoa wito wa kuhakikisha ushiriki...
Image
TATHIMINI YA KINA JUU YA MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA, UKIFAFANUA MJADALA MZIMA JINSI WADAU WALIVYOTOA NA KUCHANGIA MAWAZO YAO JUU YA MADA ILIYOWEKWA MEZANI  (SIKU YA KWANZA) Mkutano ulilenga kuimarisha demokrasia na kuleta maridhiano kati ya vyama vya siasa. Kauli mbiu ya mkutano ilikuwa "Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia." Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na wadau katika mkutano huo ni pamoja na dhana ya R4 (Reconciliation, Resiliency, Reforms, Rebuilding), misingi ya kutengeneza dira, na nafasi ya R4 katika kuleta utendaji mzuri wa hali ya kisiasa.     Watoa mada walisisitiza umuhimu wa maridhiano na uelewa wa pamoja kati ya vyama vya siasa, na kueleza kuwa tofauti za kiitikadi hazipaswi kuvunja umoja wa nchi. Pia, walijadili misingi ya kutengeneza dira, ikiwa ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, kujenga upya, kuvumiliana, kusameheana, na maridhiano.   Watoa mada walisisitiza pia umuhimu wa kufanya marekebis...
Image
  NINI NAFASI YA SERIKALI, ASASI ZA KIRAI,  VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HIZI R4 NA NINI  KIFANYIKE Bw. Salim. Niliposema 'reform’ sikuwa na maana tuanze na reform. Hivyo ni lazima tuanze na maridhiano na kuvumiliana. Nakubaliana na wote wanaosema kuwa R4 ni falsafa sahihi sana. Hii mimi ninaamini kuwa hii itakuwa ni ‘legacy’ kwa mama Samia. Nini kifanyike, tuione Serikali ikifanya kwa vitendo, hili sio suala la kisiasa. Tunaona mabadiliko kwenye mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali. Ingawa kwenye siasa kuna mkwamo kwenye Sheria za Uchaguzi na Katiba mpya. Asasi za kiraia ziwaeleze wananchi na kuwafundisha.     Bw. S.Wasira. Vyombo vya Habari vifanye kazi yake ya kuelimisha umma kwakuwa vinasilikizwa na Wananchi. Nafasi ya Serikali ni haya yanayoendelea, Serikali iko kwenye usahihi. Tutazame ‘reforms’ kwenye maeneo yote kwa mfano elimu,  vyama vya siasa vina nafasi ipi. Bw. Ado - ACT WAZALENDO. Mchakato wa Katiba nchi siyo jambo la kusubiri, mchakato wa Kat...
Image
UFAFANUZI WA 4R KUTOKA KWA  WADAU MBALIMBALI KATIKA MREJESHO WA  MKUTANO WA MSAJILI  WA VYAMA VYA SIASA   Bw. Doyo. Naomba nianze na nia ya Mhe.Rais, nianze na Watendaji wa chini. Serikali itengeneze programu maalum yakuwafanya hawa Watumishi wa Serikali wazielewe vizuri R4. Dira ya Taifa ikieleweka tutapata Wawekezaji pia. Mhe. Rais anasisitiza kusikilizana na kutuvumilia. Hivyo kuna umuhimu watendaji wawe na uelewa.   Bw. Salim Kwa kiwango gani R4 zinaweza kuisadia kuendana na Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda za 2063. Haya yote yanapaswa yaangaliwe na nguzo za kidunia, ili dunia itupime hivyo. Kama kuna joto kubwa la kisiasa hautaweza kufikia kwenye haya maendeleo.  Reforms zinazozungumzwa hapa ni pamoja na kuvumiliana kwa hoja ilituweze kuitengeneza nchi yetu, tunapaswa kuja na reforms za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivyo tuweze kupimana kwa uvumilivu na ukweli.   Bw. Ado Said Falsafa hii ikitekelezwa kwa ukamilifu basi tutaenda sambasamba n...
Image
UFAFANUZI WA 4R KAMA  ULIVYOONGOZWA NA  BW. ABBAKARI  MACHUMU MWONGOZA MADA (SIKUYA 01) Wachochea Mada walipata nafasi kusisitiza mambo  yafuatayo Dhana ya R4 Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resiliency), Mabadiliko (Reforms), Kujenga Upya (Rebuiling), uelewa wa jumla wa watoa mada ulikuwa washiriki asilimia 80%.  Ilisisitizwa kuwa tofauti zetu za kiitikadi zisivunje umoja wetu kama nchi.   Misingi ya kutengeneza dira Uhuru wa vyomba vya habari na Uhuru wa Kujieleza, kujenga upya, kuvumiliana, kusameheana na maridhiano.   Kurudishwa kwa vikao vya kisiasa, utendaji wa Jeshi la Polisi umebadilika, na sasa tunaweka misingi thabiti. Kuna mambo yakuweka mifumo ya kisiasa, uchaguzi na demokrasia. Dira ya umoja inayounganisha taifa. Changamoto zetu za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kidemokrasia visijirudie. Kwa hivi sasa tunasahihisha yale yaliokuwa yametokea huko nyuma. Nyenzo inayotuongoza ni uchambuzi wa kimuktadha (contextual analysis), jawa...
Image
  MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA   NCHINI, UKIJADILI   NA KUPOKEA MAONI YA MSWADA WA SHERIA ZA   UCHAGUZI NA SHERIA ZA VYAMA VYA SIASA.  Baraza la Vyama vya Siasa nchini liliandaa Mkutano Maalum wa kujadili na kupokea maoni ya Wadau juu ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa ambayo ni matokeo ya mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mgeni Rasmi katika mkutano huu alikuwa Bw. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wadau na Washiriki walijulishwa na kuhusu lengo la Mkutano, pamoja na mambo mengine, ilielezwa kuwa ni Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaojadili na kupokea maoni ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa  Kauli mbiu ya mkutano huu Ilikuwa ni “ Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia ”. Mara baada ya maelezo haya. Mkutano huu uliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera...
Image
MKUTANO HUU UMEKUWA WENYE TIJA KWANI MMETOA MAONI KWA KUZINGATIA MASLAHI MAKUBWA YA NCHI YETU - MHE. DOTO BITEKO Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaungana na watu wengine waliosema hapa nami nitoe shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa Juhudi zake ameweza kuimarisha ustawi wa Demokrasia hapa nchini sambamba na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuwaletea maendeleo Watanzania" "Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amekuwa mfano wa kuigwa kitaifa na kimataifa kuhakikisha Demokrasia yetu inazidi kustawi na kuifanya Demokrasia yetu kuendeshwa kwa misingi ya haki, utawala bora na kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea na bila kusahau mazingira ya watu ambao bila wao Serikali haipati uhalali" "Mkutano huu umekuwa wenye tija na mimi nimekuwa nikiufuatilia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mmezungumza mengi kutokana na Ajenda mlizomuwa nazo na ni wazi kabisa wadau waliokuwa wengi wametoa maon...