UPI MSINGI WA KATIBA YA NCHI? LAZIMA IANZE NA NENO "SISI” TUMEAMUA ~ DR...
Hii maana yake ni mamlaka ya wanachi kuamua ni namna gani wanapaswa waongozwe na Maisha Yao yaweje kwa hiyo Katiba sio suala la kupuuza na imetajwa kama msingi wa katiba ya sasa ya mwaka 1977 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________ Sheria ya 1984 Na.15 ib.3 KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 UTANGULIZI MISINGI YA KATIBA KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani: NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu: KWA HIYO, BA...